img

Wananchi Songwe watakiwa kuendelea kuboresha miundo mbinu ya matundu ya vyoo kuepuka magonjwa kwa watoto

December 6, 2020

Na  Baraka Messa, Songwe.

KATIKA kuhakikisha kuboresha mazingira mazuri ya kujifunzia na kuwaepusha Wanafunzi kupata magonjwa ya Mlipuko, Wananchi katika Mkoa wa Songwe wametakiwa kuendelea kuboresha miundo mbinu ya vyoo katika kipindi hiki Cha mvua nyingi katika shule zote zenye upungufu.

Akizungumza na gazeti hili afisa elimu Mkoa wa Songwe Juma Kaponda alisema pamoja na changamoto ya vyoo kuripotiwa mara kwa Mara na Vyombo vya habari Serikali ikishirikiana na Wananchi wamefanikiwa kwa kias kikubwa kupunguza changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Alisema katika miezi ya agost, septemba na octoba jumla ya matundu ya vyoo 500 katika shule 28 ambazo zilikuwa na upungufu   yamekamilika na kupunguza changamoto hiyo.

Alisema miundo mbinu ya vyoo ni muhimu Sana hasa kipindi hiki cha mvua ambapo ubora na uwepo wa vyoo vya kutosha huepusha Wanafunzi kupata magonjwa ya Mlipuko.

Alisema kuna baadhi ya maeneo bado Wananchi wanachangia mambo ya siasa na kupelekea miundo mbinu ya vyoo, madawati na madarasa kutokamilika kwa muda mwafaka hivyo kupelekea watoto kujifunzia katika mazingira magumu.

“Shule zote za Msingi za Seriikali katika maeneo yote nchini ni Mali ya mitaa na Vijiji, na shule zote za Sekondar nchini ni Mali ya Kata , Hivyo Wananchi walitambue Hilo  kazi ya Serikali ni kuja kumalizia tu baada ya wao kuunza na kufikia kiwango Cha rinta” alisema Kaponda.

Kuhusu watoto wa awali Kaponda alisema kuwa wanahitaji miundo mbinu mizuri zaidi ya kujifunzia yenye dhana muhimu za kujifunzia.

Mkurugenzi wa Halmashaur ya Mbozi Hanji Godigodi alisema kuelekea kipindi hiki Cha mvua amewaagiza wakuu wa shule wakisaidiana na Viongozi wa Kamati za shule kuhakikisha wanakamilisha ujenzi mbalimbali  kuwanusuru watoto kupata magonjwa ya Mlipuko.

Kwa upande wake Kaim afisa afya Wilaya ya  Mbozi Togolai Gembe akiongea na Mwaandishi wa gazeti hili alisema kipindi Cha mvua huwa kunatokea magonjwa mengi ya Mlipuko na magonjwa ya tumbo huwa yanayotokea kutokana na uchafu wa mazingira na kukosekana vyoo Bora.

Aliongeza kuwa watoto wadogo hasa chini ya miaka mitano kipindi Kama hiki wanahitaji ulinzi wa karibu ili kuhakikisha wanakuwa salama.

“Msimu wa Mvua pia ndio msimu wa matunda hivyo ni vizuri kuhakikisha watoto wanahakikishiwa mazingira Safi kuepuka kupata magonjwa ya tumbo kutokana na kunywa maji ambayo sio salama na matunda bila kuoshwa” alisema Gembe.

Alisema kuna baadhi ya jamii bado hazijajua umuhimu wa kuwa na vyoo bora hali inayopelekea kujisaidia vichakani na kuhatarisha afya zao kutokana na kinyesi kuzolewa na maji baada ya mvua kunyesha na kutawanywa sehemu mbalimbali mpaka kwenye vyanzo vya maji.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *