img

Wakazi Kibindu kuondokana na shida ya maji

December 6, 2020

Na Omary Mngindo, Kibindu

WAKAZI wa Vijiji vinavyounda Kata ya Kibindu jimbo la Chalinze, Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wanataraji kuondokana na changamoto ya maji iliyowakabili kwa muda mrefu.

Hayo yamo katika taarifa ya James Kionaumela Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mzingira Vijijini (RUWASA), katika ziara katika vijiji vya Kibindu, Kwamduma, Kwamsanja na Kwakonje, chini ya Mkuu wa wilaya Zainab Kawawa na Mbunge Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.

Taarifa ya Kionaumela imeeleza kuwa, utekelezaji wa miradi hiyo Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 kwa ajili ya miradi hiyo, ambapo milioni 700 kwa ajili ya Bwala la Kijiji cha Kwamsanja, wakati Kijiji cha Mjembe kikitengewa milioni 900

“Kijiji cha Kibindu kina wakazi 11,154 wanapata maji kupitia mradi uliofadhiliwa na JIC mwaka 2009, vyanzo vyake visima viwili kila kimoja kina uwezo wa kutoa lita 6,000 kwa saa, unatumia Jenereta mbili una vituo 20 huku wateja 40 wameunganishiwa watu 10,238,” ilieleza taarifa hiyo..

Imeongeza kuwa upanuzi wa mradi utaongeza mtandao wa bomba lenye urefu wa mita 830 kuelekea Vulala, shule ya Sekondari Kibindu na ujenzi wa vituo viwili vya kuchotea maji, na ufungaji wa pampu ya kutumia nguvu ya jua sanjali na ujenzi wa tenki dogo lenye ujazo wa lita 22,000.

“RUWASA kushirikiana na Wataalamu kutoka Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu wamefanya upimaji hali ya upatikanaji wa maji ya chini ya ardhi, taarifa ya awali imewasilishwa na kuainisha maeneo ya uchimbaji wa visima, hatua inayofuata ni uchimbaji ili kupata vyanzo vya huduma,” ilieleza sehemubya taarifa ya Kionaumela.

Kwa upande wake Kawawa ameishuluru Serikali kwa kuweka kipaumbele katika mirafi ya maji ambayo ndio changamoto kubwa, huku akiwataka viongozi wa RUWASA kutekeleza majukumu yao mapema ili kazi hizo zikamilike hatimae wanancji wanufaikea na huduma.

“Wakatu anazungumza na Taifa kupitia ufunguzi wa bunge, Rais Dkt. John Magufuli alisema kuwa Serikali yake itaendelea kuelekeza nguvu katika kutatua kero za wananchi, hususani sekta ya maji, leo tunashuhudia kazi inayofanyika, niwaombe hii kazi ikamilike mapema,” alisema Kawawa.

Nae Ridhiwani alisema kuwa adha ya maji katika vijiji vinavyounda Kata ya Kibindu ilikuwa kubwa, na kwamba pamoja na uwepo wa mikakati hiyo wananchi walikuwa wanalalamikia ujenzi wa mabwawa hayo, lakini amepata faraja kubwa kuona RUWASA wakiwa katika harakati hizo.

“Wananchi wetu wa Kata ya Kibindu kwa muda mrefu walikuwa wanasubiri ujenzi wa mabwawa haya kwa ajili ya upatikanaji wa maji, leo nimefarijika sana kuona mikakati iliyopo ya kuwaondolea adha ya maji wananchi hawa,” alimalizia Ridhiwani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *