img

Raia wa Ubelgiji waandamana kupinga ubaguzi na shinikizo za polisi

December 6, 2020

Maandamano ya kupinga ubaguzi na shinikizo za polisi yaliandaliwa katika mji mkuu wa Brussels nchini Ubelgiji.

Takriban watu 150 walikusanyika katika mji mkuu wa Brussels kwa ajili ya maandamano ya kupinga ubaguzi na shinikizo za polisi.

Waandamanaji walikusanyika mbele ya jengo la baraza la Jumuiya ya Ulaya (EU) wakiwa wamebeba mabango na kutoa kaulimbiu dhidi ya ubaguzi.

Waandamanaji hao waliopinga shinikizo za polisi zilizoongezeka Ubelgiji na Ufaransa, pia walikosoa mazungumzo ya kanuni mpya ya usalama huku wakitoa wito wa kujiuzulu kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. 

Maafisa wa polisi walishika doria na kuchukuwa hatua kali za kiusalama katika barabara zinazoelekea kwenye eneo la maandamano. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *