img

Msuva atambulishwa Wydad Casablanca, apewa namba 11

December 6, 2020

Mtanzania Simon Msuva jana alitambulishwa na klabu yake mpya ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco na kukabidhiwa jezi namba 11 na sio 27 kama tulivyomzoea au 12 anayoitumia timu ya taifa.

Msuva ameeleza amechukua jezi hiyo baada ya kukuta jezi namba 27 ina mtu lakini 11 ndio namba yenye historia nyuma ya pazia, Msuva amesema amechukua jezi namba 11 kama heshima kwa mchezaji wa zamani wa Simba SC Musa Mgosi ambaye aliwahi kumuona akiwa mtaani akicheza na kumwambia atafika mbali ana uwezo mkubwa sana.

“Aliyefanya niipende zaidi namba 11 ni Musa Hassan Mgosi watanzania wengi labda walikuwa hawafahamu mimi shabiki mkubwa wa Mgosi, aliwahi kuniona Sinza kwenye mechi za mtaani nikicheza na timu ya mtaani kwake”

“Alisikia kuwa kuna kijana anaitwa Simon anajua sana mpira ndio akataka anione, alivyoniona kuna maneno akaniambia wewe kijana unajua sana mpira lazima utafika mbali na alinipa zawadi ya jezi yake namba 11 ya Simba nikawa naenda nayo kwenye Ndondo”>>>.Msuva

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *