img

Msomali afikishwa Mahakamani kwa kusafirisha binadamu

December 6, 2020

Mtu mmoja raia wa Somalia amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu mkazi kisutu kwa kosa la kuwasafirisha raia saba wa Ethiopia kupitia mpaka wa Namanga Longido jjijini Arusha kwenda nchi za Kiarabu.

Raia huyo Ateyb Isamail Yusuph amesomewa mashitaka yake na Wakili wa Serikali Kija Luzungana mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo Augustina Mbabdo ambaye amedai mshitakiwa huyo ametenda kosa hilo Agost 19, 2020 akiwa katika  mpaka wa Namanga Jijijini Arusha kabla ya kukamatwa nakufunguliwa mashtaka katika mahakama ya Mkazi Arusha.

Aidha mshitakiwa huyo amekana Mashitaka yanayomkabili ambapo ameeleza mahakama hiyo kuwa hajawahi kujihusisha na biashara haramu ya kusafirisha binadamu zaidi ya familia yake.

Hata hivyo Wakili Kija Luzungana ambaye amesoma hati Mashitaka mbele ya Hakimu Mwandamizi Augustina Mbabdo amedai upelelezi wa shauri hilo bado kukamilika hivyo kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa Hadi Decemba 17 mwaka huu na mshitakiwa amepelekwa gerezani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *