img

Mkenge awapongeza Jafo, Ulega na Kipanga

December 6, 2020

Na Omary Mngindo, Bagamoyo

MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Muharami Mkenge, amewapongeza Wabunge wenzake Suleiman Jafo (Kisarawe), Abdallah Ulega (Mkuranga) na Kipanga Juma (Mafia) kwa kuteuliwa nafasi za Uwaziri na Unaibu Waziri.

Aidha Mkenge amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa uteuzi huo wa wana-Pwani hao, hatua inayoonesha kukubalika katika nafasi hizo huku pongezi za kipekee akizipeleka kwa Jafo, kwa namna alivyoitumikia Wizara hiyo miaka mitano iliyopita.

“Miaka mitano iliyopita Jafo ameitendea haki Wizara hiyo hivyo Rais amteue tena kuiongoza, Ulega Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo kutoka Mifugo na Uvuvi, Kipanga ameteuliwa Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, tuna imani na Mawaziri hao,” alisema Mkenge.

Alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli kuendelea kumkabidhi Wizara ya TAMISEMI Jafo, kumetokana na namna alivyoitendea haki katika kipindi kinachoishia mwaka huu wa 2020, kutokana na alivyofanyakazi kubwa kwenye kipindi hicho.

“Nikiwa mwakilishi wa wana-Bagamoyo nitumie fursa hii kumshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa Baraza zuri aliloliunda litalofanyakazi kipindi kinachokuja, lakini kipekee niwapongeze Jafo, Ulega na Kipanga kuaminiwa kwenye Baraza hilo,” alisema Mkenge.

Aliongeza kuwa kuteuliwa kwa wabunge hao kushika wadhifa huo imekuwa faraja kwa wana-Bagamoyo kwani watawatumia katika kupambana na changamoto zinazowakabili kwenye sekta husuka, hivyo kwao ni jambo la kumshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa uteuzi huo.

“Wana-Bagamoyo tunaendelea kumuombea dua Rais wetu Dkt. Magufuli, kwani tangu achaguliwe mwaka 2015 amefanya mambo mengi makubwa, tunaimani kwamba awamu hii atatutumikia sanjali na kutuondolea kilio cha barabara ya Makofia Mlandizi kama alivyoahidi,” alimalizia Mkenge.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *