img

Mhandisi Nyamhanga atoa miezi mitatu kukamilika kwa jengo la upasuaji, Kilolo

December 6, 2020

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga ametoa miezi mitatu kwa Mkandarasi PACHA Building construction kukamilisha ujenzi wa Jengo la Upasuaji ifikapo Februari, 2021 

Mhandisi Nyamhanga ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya hiyo Mkoani Iringa. 

Amesema kuwa Hospitali hiyo kwa sasa imekamilika na imeanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje, lakini bado kuna baadhi ya majengo ambayo ujenzi wake haujakamilika jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za Serikali za kuhakikisha huduma zote za afya zinapatikana karibu na wananchi

Akifafanua zaidi amesema kuwa mkadarasi huyo aliwasilisha hati za malipo tatu na tayari Serikali ilishalipa hati mbili, hivyo anawajibu wa kuhakikisha Jengo hilo linakamilika kwa wakati uliopangwa ili lianze kutoa huduma kwa jamii.

“Hakuna sababu ya mkandarasi kusimamisha ujenzi, kwa kuwa serikali imeshalipa baadhi ya fedha, naagiza mkandarasi Pacha Buildingi Construction kuhakikisha anamaliza ujenzi ili wananchi wa Kilolo waweze kupata huduma ya upasuaji katika Hospitali hiyo” amesisitiza Mhandisi Nyamhanga

Wakati huo Mhandisi Nyamhanga Aidha. ameuagiza  uongozi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kuhakikisha wanasimamia kikamilifu   ujenzi wa  majengo yaliyobaki  katika  Hospitali ya Wilaya ya Kilolo ili iweze kutoa huduma  kwa jamii.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kituo hicho Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo  Dkt Mohamed Manguna  amesema  mradi umegarimu zaidi ya shilingi  bilioni 4.3 ambapo Serikali imetoa  zaidi ya shilingi bilioni 4, wadau wa maendeleo shilingi milioni 37 na  zaidi ya shilingi  milioni 336  zimetolewa  na Halmashauri hiyo  kutoka katika mapato ya ndani.

Aidha, Dkt. Manguna  amesema kuwa kukamilika  kwa ujenzi  wa Hospitali  hiyo kutawezesha   Halmashauri kukabiliana  na magonjwa  ya kuambukiza, kupunguza  kiwango cha magonjwa  na vifo vya watoto wachanga na vifo vya mama wajawazito  kupunguza uhitaji mkubwa wa huduma za rufaa  hasa kwa akinamama wajawazito na watoto  na  kukabiliana  na uhitaji  mkubwa  wa huduma za dharura za upasuaji Mkubwa na mdogo unaotokana na ajali  za vyombo vya moto.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *