img

Maelfu ya watu wameondolewa baada ya bomu la vita vikuu vya II vya dunia kugundulika mjini Frankfurt

December 6, 2020

Takribani wakazi 13,000 wa jiji la kibiashara la Ujerumani, Frankfurt waliondolewa kutoka kwenye makaazi yao Asubuhi ya leo, kupisha uteguaji wa bomu la kilo 500, la wakati wa Vita Vikuu vya II vya dunia. Bomu hilo la majeshi ya Uingereza lilibainika Alhamisi katika harakati za ujenzi. 

Wale ambao hawakuwa na mahala mbadala pa kuishi, walipangiwa eneo la kujihifadhi kwa muda katika ukumbi wa mikutano mjini Frankfurt. 

Maeneo ambayo yalipaswa kutengwa kutokana na kitisho cha bomu hilo ni pamoja na nyumba za kuwahifadhia wazee, mifumo mabomba ya gesi ya vipasha joto majumbani, vituo vya mtandao wa intaneti na treni. Kulitarajiwa pia kuwepo ucheleweshaji wa safari za treni za masafa mafupi na marefu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *