img

Maandamano ya dhidi ya Netanyahu Israel

December 6, 2020

 

Watu 27 wameripotiwa kuwekwa kizuizini na maafisa wa polisi kwenye maandamano ya kumpinga Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu yaliyoandaliwa nchini Israel. 

Katika taarifa iliyoandikwa na idara ya polisi ya Israel, iliarifiwa kuwa maandamano ya kumpinga Netanyahu yaliandaliwa kwenye eneo la Paris Square lililoko karibu na Jerusalem Magharibi. 

Katika taarifa hiyo, iliandikwa,  “Watu 27 wamekamatwa kwenye maandamano yaliyosababisha kufunga barabara za eneo la Paris Square na kuvuruga utulivu wa umma.”

Kulingana na vyombo vya habari vya Israel, wananchi wameandaa maandamano katika maeneo mbalimbali ya nchi hasa mjini Jerusalem na Tel Aviv, ili kumtaka Netanyahu ajiuzulu kutokana na kashfa ya ufisadi na uongozi mbaya wakati wa janga la corona (Covid-19) nchini humo. 

Taarifa zaidi zimefahamisha kwamba maelfu ya watu walishiriki kwenye maandamano yaliyoandaliwa Jerusalem ambapo mara kwa mara maafisa wa polisi  walikabiliana nao.

Kwa upande mwingine, raia mmoja wa Israel kwenye umri wa miaka 82 aliyeshiriki maandamano ya Tel Aviv, alijeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na gari la mtu mwengine anayeunga mkono serikali, na baadaye akapoteza maisha alipokuwa hospitalini.

Katika taarifa hizo, ilibainishwa kwamba mtu aliyepoteza maisha ni Dror Soffer, babake Adi Soffer Teeni ambaye ni Mkurugenzi wa Facebook kwa nchi ya Israel. 

Katika nchi ya Israel ambayo imeathirika kwa wimbi la pili la Covid-19 na ongezeko la ukosefu wa ajira, kumekuwa na maandamano kwa kipindi cha miezi 5 yanayoandaliwa ili kumtaka Netanyahu ajiuzulu kutokana na “uongozi mbaya wakati huu wa janga na kashfa ya ufisadi.”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *