img

Henrietta Lacks: Seli pekee za mwanadamu zilizoendelea kukua na kuzaliana katika maabara

December 6, 2020

Dakika 4 zilizopita

1940s photo made available by the family shows Henrietta Lacks

Maelezo ya picha,

Simulizi yake ilikuwa maafuru kutokana na kitabu kilichokuwa na mauzo mazuri mwaka 2010 ‘The Immortal Life of Henrietta Lacks’

Ni kidogo sana katika historia wanaoweza kusemekana kwamba walinusuru maisha ya wengi ikilinganishwa na Henrietta Lacks.

Msichana Mmarekani mweusi ambaye anahaki ya kudai kuwa amechangia pakubwa katika sekta ya matibabu – bila hata ya yeye mwenyewe kujua.

Watafiti walibaini kwamba ndio mwanadamu wa kwanza ambaye seli zake zinaweza kukua na kuzaliana zikiwa katika maabara.

Na historia hiyo ndio ikawa mwanzo wa matibabu ya tiba chungu nzima.

Familia ‘iliachwa gizani’

Henrietta Lacks aligundulika na saratani ya tumbo la uzazi isiyoweza kupona mwaka 1951 akiwa na umri wa miaka 31, muda mfupi tu baada ya kujifungua mtoto wake wa tano.

Wakati huo hospitali nyingi Marekani bado zilikuwa zinaendeleza unyanyapaa kati ya watu weusi na wazungu kwahiyo kulikuwa na machaguo kidogo sana kwake yeye ya kupata matibabu punde baada ya kuanza kuonesha dalili za ugonjwa huo.

Wakati huo aliamua kwenda hospitali ya Johns Hopkins huko Baltimore, Maryland, kwasababu ilikuwa karibu na nyumbani kwake.

Cha ajabu ni kwamba, seli za uvimbe aliokuwa nao zilichukuliwa akiwa hospitalini bila ya ridhaa yake.

Na seli hizo ndiyo zilichangia maendeleo makubwa tu katika upatikanaji wa chanjo, matibabu ya saratani na hata tiba kwa wenye ugumba kulikotokana na tafiti zisizopungua 75,000.

July 2013 photo shows a researcher placing HeLa cells in an incubator at at the US National Cancer Institute

Maelezo ya picha,

Seli za Lacks zilifanya maajabu ambayo hayakuwa yamewahi kuonekana kabla – zilikuwa hai na kuendelea kukua

Familia ya mwanamke huyo ambaye seli zake zimeleta mapinduzi katika nyaja ya tiba ilikuja kujua vile seli za mpendwa wao zinavyotumika, miaka 60 baada ya kifo chake.

Familia hiyo ilijua ukweli sio kwamba seli za mpendwa wao zilichukuliwa tu lakini pia zilikuwa zimesambazwa katika maabara mbalimbali kote duniani pale mwanasayansi mmoja alipowasiliana nao mwaka 1973 kuomba sampuli ya damu.

Hadi kufikia sasa, majaribio ya kukuza seli za mwanadamu nje ya mwili wake bado hazijafanikiwa. Lakini mapinduzi yaliyopatikana ni kwasababu ya Henrietta Lacks.

Tofauti na seli zingine za mwanadamu ambazo zimewahi kupelekwa katika maabara, seli za Lacks ziliendelea kukua na kuzaliana hadi hii leo na zinasaidia katika uchunguzi na mchakato wa kuendelea kutafuta tiba.

Kawaida, seli za mwanadamu zinaweza kujigawanya hadi mara 50 kabla ya kushindwa kufanya hivyo.

Lakini seli za Lacks ni tofauti kwasababu zinaweza kujigawanya na kuzaliana bila kukoma.

Mamilioni ya watu wameishi muda mrefu kwasababu ya seli zake – ambazo pia zimetumika kutengeneza chanjo ya kwanza ya polio, dawa za saratani na vitamin.

Familia yake haikuwahi kujua kwamba amechangia seli hadi pale mwanahabari Rebecca Skloot alipofuatilia tena uchunguzi wa vinasaba vyake miaka 60 baadaye.

Jeri Lacks Whye, mjukuu wake, anasema familia yao “iliachwa gizani” kuhusu tafiti zilizokuwa zinafanyika.

“Tunafuraha kuwa sehemu ya majaribio yanayoendele,” alizungumza na shirika la habari la Associated Press.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *