img

Hakimu kizimbani kwa madai ya kutaka kumtoa mfungwa gerezani

December 6, 2020

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mbeya imemfikisha mahakamani hakimu mkazi wa  mahakama ya Mwanzo Igurusi wilayani Mbarali mkoani Mbeya, Harrison Makinda kwa tuhuma za kufanya udanganyifu ili kumtoa mfungwa gerezani.

 Akizungumza leo Jumamosi Desemba 5, 2020 mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mbeya, Julieth Matechi amesema hakimu huyo anakabiliwa na kesi namba 272/2020 ya kutoa taarifa za uongo za mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha sheria 122 na kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu.

Matechi amesema katika shtaka la kwanza Makinda  anadaiwa Mei 16,  2019 aliwasilisha nyaraka yenye maelezo ya uongo kwa ofisa wa gereza la Rujewa wilayani Mbarali akimtaarifu kwamba mshitakiwa (jina limehifadhiwa) aliyetiwa hatiani na kutumikia kifungo cha miaka mitano jela anatakiwa kutolewa  gerezani.

Amesema  kuwa hakimu huyo alidai mshtakiwa  anatakiwa kulipa faini ya Sh100,000 na fidia ya Sh600,000 ili atoke gerezani wakati  akijua wazi kuwa si kweli na kwamba  hukumu aliyoandikiwa mshtakiwa haikuwa na adhabu ya faini hiyo.

Hakimu huyo alikana mashtaka na kuachiwa kwa dhamana huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Januari 20 ,2021.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *