img

Chombo kilichobeba mawe kutoka anga ya mbali chatua salama

December 6, 2020

Dakika 6 zilizopita

A team member carries the capsule, which contains samples from an asteroid

Maelezo ya picha,

Timu ikibeba chombo chenye sampuli za asteroidi

Chombo kilichobeba mawe kutoka kwa sayari ndogo yaani asteroidi kiko sawa, kulingana na wanasayansi.

Chombo kilichobeba mawe hayo kutoka kwa jiwe la kwenye anga ya mbali katika sayari ndogo yaano asteroid kwa jina Ryugu, kimeshuka vizuri karibu na eneo la Woomera kusini mwa Australia Jumamosi jioni saa za eneo hilo(GMT).

Timu ya wanasayansi wa Australia imebaini chombo kutoka anga za mbali juu ya ardhi yake huku parachuti iliyotumika katika safari hiyo ikitua juu ya mti.

Capsule

Maelezo ya picha,

Parachuti iliyotumika katika safari hiyo ikiwa juu ya mti

Sampuli hiyo ya mawe awali kabisa ilichukuliwa na chombo cha anga cha Japani cha Hayabusa-2.

Chombo cha Japani kilitumia zaidi ya mwaka mmoja kuchunguza sayari ndogo ya Ryugu kabla ya kurejea duniani.

Wakati kinawasili katika sayari yetu, Hayabusa-2 iliachilia chombo cha Ryugu kilichokuwa na mawe hayo adimu kutoka anga za mbali na injini yake ikaungua na kuelekea upande mwingine.

Hatahivyo, chombo cha Ryugu kilifanikiwa kuingia katika anga la dunia.

Capsule in its protective box

Maelezo ya picha,

Chombo hicho kimechukuliwa kwa kutumia kasha maalum kama inavyoonekana kwenye picha

Fireball from capsule

Maelezo ya picha,

Kamera za Australia ilifanikiwa kunasa mng’ao wa tufe la moto wakati kinaingia katika anga la dunia

Mtandao wa Twitter wa maafisa wa chombo cha Japani cha Hayabusa-2 walisema chombo hicho na parachuti yake vimepatikana saa moja na dakika 47 usiku.

“Tumechukua chombo hicho chenye hazina muhimu,” mkuu anayesimamia safari hiyo Dkt. Yuichi Tsuda alisema.

Aliongeza kuwa hakuna kilichoharibika.

Dkt. Hitoshi Kuninaka, mkuu wa Taasisi ya Anga za Mbali Japani alisema: “Tulianza kuunda chombo Hayabusa-2 mwaka 2011. Na sasa ndoto yetu imetimia.”

Safari itakayofuata itajumuisha chombo kwa jina MMX, ambacho kitalenga kuleta sampuli kutoka mwezi mkubwa katika sayari ya Mihiri unaojulikana kama Phobos.

Ryugu

Maelezo ya picha,

Chombo kilichotumiwa na Hayabusa-2 kilirejesha picha hii inayoonesha hali ilivyo katika sayari ndogo yaani asteroidi ya Ryugu

Chombo cha anga cha Hayabusa-2 ambacho kilipita dunia baada ya kuachilia chombo kilichokuwa kimebeba mawe hayo kutoka anga za mbali kitatumwa tena katika safari nyingine ambayo ni kwenye asteroidi ndogo zaidi kuliko ya Ryugu na kutarajiwa kufika huko mwaka 2031.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *