img

Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara imezindua rasmi oparesheni ijulikanayo kama ondoa mapori

December 5, 2020

   

Na Hamisi Nasri, Masasi 

  WILAYA ya Masasi mkoani Mtwara imezindua rasmi oparesheni ijulikanayo kama ondoa mapori ongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara lengo likiwa ni wilaya iwe na chakula cha kutosha kwa wananchi wake lakini pia kuwa na mazao mengi ya biashara

   Mkakati huo umezinduliwa jana mjini katika mkutano maalumu uliowakutanisha wadau mbalimbali wa kilimo,uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa halmashauri ya wilaya ya Masasi ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa wilaya hiyo,Selemani Mzee.

   Akifungua mkutano huo,mkuu huyo wa wilaya,Mzee alisema mpango huo ni utekelezaji wa agizo la mkoa la kila wilaya ijiwekewee mpango wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na yale ya biashara.

    Mzee alisema wilaya ya Masasi hivi imeshajipanga kuona inaongeza hali ya chakula ndani ya eneo lake jambo hilo litasaidia kuzifanya kila kaya kuwa na chakula cha kutosha na kwamba mpango huo utafanikiwa iwapo kila mmoja atakuwa anashiriki katika kilimo hasa kuwa na shamba.

    Alisema kupitia mkakati huo wilaya ya Masasi wa kuwa na operesheni ya uzalishaji mazao mbalimbali yanayostawi katika kila eneo la halmashauri kwa kuhakikisha kuwa katika kila eneo linalofaa kwa kilimo yanatumika ipasavyo.

  Alieleza kuwa kupitia mpango huo uhamasishaji vijana kushiriki katika shughuli za kilimo ni lazima ufanyike hasa kwa vijana ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi katika kuaa vijiweni vijana hao wakishirikiipasavyo katika kilimo lengo la kuongeza hali ya chakula itafikia malengo.

  Mzee alisema iwapo mapori ambayo yametekelezwa yakianza kutumika kwa kilimo Masasi itakuwa na uzalishaji mkubwa wa chakula na hata hali achakula ndani ya kaya pia itakuwa ya kiwango cha kuridhisha.

   “Uhamasishaji huu ufanyike kwa vijana wote ambao wanakaa vijiweni bila ya kazi kuanzia kwa sasa kila kijana lazime awe na shamba lengo ni kuongeza uzalishaji wa chakula hivyo kamati zitakazoundwa zikafanyike kazi hii kwa umakini,”alisema Mzee 

  Akifananua kuhusu mpango huo na kuainisha vipaumbele vya mkakati huo, afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Masasi, Reinfred Tamba alisema hatua ya kwanza ni kuunda kamati za hamasa za kuondoa mapori, kamati hizo zitakuwa katika ngazi mbili ngazi ya wilaya na kata.

   Alisema moja ya majukumu ya kamati hizo ni pamoja na kubainisha mashamba yote ambayo yametekelezwa ikiwemo mashamba ya mikorosho,kubainisha mashamba ya mikorosho isiyo zaa na iliyo zeeka.

   “Mkakati huu pia utabaini mapori yaliyotekelezwa kisha kuyagawa kwa vijana na jamii kwa ujumla ili yatumike kwa kilimo hasa katika kupanda mazao ya chakula na biashara ili lengo letu la kuongeza hali ya chakula na mzao ya biashata itimie,”alisema Tamba

  Naye afisa maendeleo ya jamii ambaye pia ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Masasi alisema kuwa mpango huo utasimamiwa kikamilifu hasa kuona kila kijana waliopo vijiweni wanakuwa na mashamba hatimaye kila kaya inakuwa na chakula cha kutosha.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *