img

Urusi: Chanjo dhidi ya Corona aina ya Sputnik V yatolewa

December 5, 2020

 

Urusi imeanza kusambaza chanjo aina ya Sputnik V ya ugonjwa wa COVID 19 katika kliniki zake 70 za kiafya, hii ikiwa ni chanjo ya kwanza dhidi ya ugonjwa huo kutolewa kwa umma. 

Kikosi kazi kinachoshughulikia janga la virusi vya corona kimesema chanjo hiyo ya Urusi kwanza itatolewa kwa madaktari, na wafanyakazi wengine wa afya, walimu na wafanyakazi wa kijamii maana makundi hayo ndio yalio katika hatari kubwa ya kuambukizwa. 

Urusi hii leo imerekodi idadi ya juu kabisa ya maambukizi mapya zaidi ya elfu 28,000. Idadi Jumla ya watu walioambukizwa imefikia zaidi ya milioni 2 tangu janga la corona lilipoanza. 

Vifo vitokanavyo na virusi hivyo nchini humo vimepindukia elfu 42,600.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *