img

Trump atoa tamko kwa wanajeshi wa Marekani walio Somalia

December 5, 2020

Rais wa Marekani Donald Trump ameamuru kuondolewa kwa karibu wanajeshi wote wa Marekani kutoka Somalia kufikia Januari 15, idara ya ulinzi nchini humo imesema.

Marekani ina wanajeshi wapatao 700 nchini Somalia wanaosaidia vikosi vya wenyeji kupigana na al-Shabab na wanamgambo wa Islamic State.

Maafisa wa Marekani walisema kuwa askari wengine watahamia nchi jirani, wakiruhusu operesheni za kuvuka mpaka.

Katika miezi ya hivi karibuni Rais Trump alitoa maagizo kama hayo ya kupunguza vikosi vya Marekani huko Iraq na Afghanistan.

Kwa muda mrefu ametaka wanajeshi wa Marekani warudi nyumbani na amekosoa operesheni za majeshi kuwa ya gharama kubwa na zisizo na ufanisi.

Amri ya kujiondoa – ambayo itasababisha wanajeshi kupangwa tena siku chache kabla ya Bw Trump kuondoka mamlakani – inabadilisha sera ya Waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani Mark Esper, ambaye alifutwa kazi mwezi uliopita na kuendelezwa kwa uwepo wa Marekani nchini Somalia.

Taarifa ya Pentagon imesema kwamba agizo la “kuwaondoa wafanyakazi wake nchini Somalia mapema 2021” haiashirii mabadiliko katika sera ya Marekani

“Tutaendelea kusambaratisha makundi ya wanamgambo wenye msimamo mkali ambayo yanaweza kuwa tishio kwa ardhi yetu.” Ilisema taarifa hiyo.

Wataalamu wengine wameonya kuwa kujitoa kwa Marekani kunaweza kuwapa nguvu wanamgambo katika eneo la Pembe ya Afrika.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *