img

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 05.12.2020: Samatta, Messi, Dier, Ings, Moyes, Diallo

December 5, 2020

Dakika 10 zilizopita

Mbwana Samatta anacheza kwa mkopo katika klabu ya Fenerbance ya Uturuki

Meneja wa Club Brugge Philippe Clement amesema hakutaka kumsajili Mshambuliaji wa Aston Villa Mtanzania Mbwana Samatta mbaye anacheza kwa mkopo katika klabu ya Fenerbance ya Uturuki. (Birmingham Mail)

Paris St-Germain wanatazama uwezekano wa kumsajili kiungo mchezeshaji wa Barcelona Lionel Messi, 33, msimu ujao. (ESPN)

Manchester United wanamfikiria Harvey Barnes wa Leicester, kama itawezekana awe mbadala wa winga mwenzie Jadon Sancho ,20 , anayekipiga Borussia Dortumund. (Sun)

Paris St-Germain wanatazama uwezekano wa kumsajili kiungo mchezeshaji wa Barcelona Lionel Messi, 33, msimu ujao

Mshambuliaji wa England Danny Ings,28, ametakiwa na kocha wake Ralph Hasenhuttl. kusaini mkataba mwingine wa muda mrefu katika klabu ya Southampton. (Sky Sports)

Manchester United wamefanya mawasiliano na wawakilishi wa mshambuliaji wa Barcelona Ousamane Dembele,23, kuhusu usajili wa mwezi Januari. ( Mundo Deportivo, via Manchester Evening News)

Manchester United wana matumaini ya kupata kibali cha kufanya kazi kwa ajili ya winga wa Atalanta raia wa Ivory Coast Amad Diallo ili mchezaji huyo, 18 aweze kujiunga na klabu hiyo wakati wa dirisha la usajili mwezi Januari. (Manchester Evening News)

Manchester United wanaweza kumchukua kocha wa Paris St-Germain Thomas Tuchel iwapo watamtimua Solskjaer wiki chache zijazo (Bild)

Winga wa Atalanta, Amad Diallo

Manchester City wanajiandaa kumaliza mchakato wa kumsajili kiungo wa kati Diego Rosa, 18 anayekipiga Gremio.(Manchester Evening News)

West Ham wako tayari kumpa mkataba wa muda mrefu kocha David Moyes. (Times)

Napoli wanafikiria kufanya uhamisho wa mkopo Januari kwa kiungo wa chini ya miaka 21 wa Scotland, Billy Gilmour, 19.(Il Corriere del Mezzogiorno, via Inside Futbol)

West Ham wako tayari kumpa mkataba wa muda mrefu kocha David Moyes

Arsenal wamerejesha shauku yao kwa kiungo wa kati wa Istanbul Basaksehir Berkay Ozcan, 22. (Transfermarkt, via Sun)

Mustakabali wa mchezaji wa Arsenal William Saliba bado haujulikani wakati ambapo klabu na mchezaji bado wakiwa hawajakubaliana ni wapi kiungo huyo wa kati ataelekea kwa mkopo. (ESPN, via Express)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa England na klabu ya Tottenham Eric Dier, 26, amekiri kuwa alikuwa tayari kuondoka kwenye klabu hiyo kabla ya kuhamia kwenye safu ya ulinzi. (Mail)

Wachezaji wa Arsenal walirushiana maneno ya ghadhabu baada ya kocha Mikel Arteta kukiita kikosi pamoja ili kubaini sababu za kuanza msimu vibaya.(ESPN)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta

Wakala wa Gareth Bale, Jonathan Barnett, amekuwa mwakilishi rasmi wa kiungo wa kati wa Rennes, Mfaransa Eduardo Camavinga, mchezaji huyo anahsishwa na taarifa za kuelekea Manchester United na Real Madrid. (L’Equipe)

Kocha wa zamani wa AC Milan Massimiliano Allegri amesema anataka kufundisha timu za ligi ya primia. Mkufunzi huyo wa zamani anahusishwa na taarifa za mipango ya kufundisha Manchester United au Arsenal. Amekuwa bila klabu tangu alipoondoka Juve mwaka 2019. (Times)

Juventus imekuwa ikihusishwa na taarifa za kumtaka kiungo wa kati wa Aston Villa, Douglas Luiz,22. (Tuttermercato Web, via Sport Witness)

Kocha wa Everton Carlo Ancelotti ameeleza kila anachokitarajia kutoka kwa Cenk Tosun na kusema kuwa mshambuliaji huyo wa Uturuki, 29, atakuwa na dakika nyingi zaidi uwanjani siku za usoni.(Liverpool Echo)

Cenk Tosun

Kocha wa QPR, Mark Warburton ameonesha kwamba hatafikira kuleta mshambuliaji wakati wa dirisha la usajili mwezi Januari na badala yake anazingatia nafasi ya beki wa kati. (West London Sport)

Pep Guardiola ana matumaini kuwa nahodha Fernandinho, 35, kiungo wa kati wa Kibrazili ambaye anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu, atakuwa na jukumu kubwa Manchester City kati ya sasa na msimu ujao. (Manchester Evening News)

Manchester United wana matumaini ya kupata ruhusa ya kuwakaribisha tena wapenzi wao Old Trafford kwa ajili ya mchezo wa ligi ya Primia dhidi ya Leeds baadae mwezi huu. (Telegraph)

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *