img

Suarez asababisha wafanyakazi wanne kusimamishwa kazi

December 5, 2020

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez amewaponza wafanyakazi 4 wa chuo kikuu cha Perugia nchini Italia, ambao wanashukiwa kuhusika katika udanganyifu wa Suarez kufaulu mtihani wa lugha ya kiitaliano na kupata B1 wakati hajui lugha hiyo.

Luis Suarez baada ya mambo kuwa magumu FC Barcelona alikuwa anataka kuhamia Juventus ya Italia lakini walikuwa washamaliza nafasi za kusajili wachezaji wanaotoka nje za nchi za jumuiya ya umoja wa Ulaya.

Suarez ndipo akalazimika kuomba uraia wa Italia na kutakiwa kufanya mtihani lakini inaonekana kama alidanganya kwani hajui hata kidogo kiitaliano na inasemekana alikuwa nao mtihani siku moja kabla licha ya kufaulu mpango wake ukakwama na kuhamia Atletico Madrid.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *