img

Papa Bouba Diop: Senegal yamuomboleza shujaa

December 5, 2020

Dakika 5 zilizopita

Pape Bouba Diop alipoichezea Senegal dhidi ya Ufaransa, 2002

Shujaa wa soka Senegal Papa Bouba Diop, aliyefariki nchini ufaransa juma lililopita akiwa na miaka 42, anazikwa kifamilia mahali alipozaliwa karibu na mji wa Dakar.

Siku ya Ijumaa, Rais Macky Sall alitoa salamu za heshima, akisema taifa limepata pigo ”kubwa”.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Papa Bouba Diop stuns France at 2002 World Cup

Diop alifunga goli pekee katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2002 walipochuana na Ufaransa.

Wachezaji wenzake kadhaa wa zamani, walihudhuria tukio hilo siku ya Ijumaa.

Walivalia T-shirt za timu ya taifa zilizoandikwa jina lake zenye namba 19.

Marion Diop, mjane wa Papa Bouba Diop akifarijiwa

Mshambuliaji El Hadji Diouf alisema Diop alisema alikuwa mchezaji wa mfano, huku Henri Camara amesema amepoteza ”pacha wake”.

Mwili wa Diop uliwasili Senegal siku ya Ijumaa ukitokea Lens, Kaskazini mwa Ufaransa. Diop alifariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.

‘Mithili ya Kabati’

President Sall said that Diop’s goal against France meant Senegal would go down in the annals of global football.

Rais Sall alisema kuwa lengo la Diop dhidi ya Ufaransa lilimaanisha Senegal ingeingia kwenye kumbukumbu za mpira wa miguu ulimwenguni.

Baada ya kuifunga Ufaransa, Senegal ilifika katika hatua ya robo-fainali. Hatua ambayo haikufikiwa na timu nyingine ya Afrika.

President Macky Sall (katikati) ameongoza shughuli za kutoa heshima za mwisho

Rais Sall ametangaza kuwa makavazi inayojengwa katika uwanja wa watu 50,000 nje ya mji mkuu, Dakar utaitwa kwa jina la Diop.

Katika safari yake ya soka Diop pia ni kushinda kombe la FA mwaka 2008 akiwa na Portsmouth. Pia aliwahi kuzichezea Fulham, West Ham United, Birmingham City na Klabu ya Ufaransa, Lens.

Aliyekuwa kocha wake akiwa Portsmouth Harry Redknapp juma lililopita aliiambia BBC kuwa alikuwa ”mtu mwenye bahati sana kumfundisha kijana bora-alikuwa wa kipekee”.

“Walimuita kabati, alikuwa na umbo kubwa kiasi cha kushindwa kumsogeza,” alisema.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *