img

Marekani kuwekea vikazwo kampuni 4 za Kichina

December 5, 2020

Marekani imetangaza vizuizi dhidi ya kampuni 4 za Kichina kwa madai kujihusisha na jeshi la China.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Idara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon), Shirika la Kimataifa la Uzalishaji la China Semiconductor (SMIC), Shirika la Mafuta la Pwani ya China (CNOOC), Kampuni ya Ushauri ya Uhandisi ya Uchina na Kampuni ya Teknolojia ya Ujenzi ya China ziliorodheshwa.

Hatua hiyo ilichukuliwa dhidi ya kampuni hizo za Kichina kwa madai ya kujihusisha na juhudi za utawala wa Beijing za kuboresha Jeshi la Ukombozi wa Wananchi nchini China.

Hatua ya kuorodheshwa kwa kampuni hizo, inamaanisha kuwa Marekani inaandaa msingi ya kisheria na kuweka vikwazo.

Kufuatia uamuzi huo, idadi ya kampuni zilizojumuishwa kwenye orodha ya vikwazo ya Marekani imeongezeka hadi kufikia 35.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying, alitoa maoni wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika mji mkuu Beijing, na kusema kwamba hatua zilizochukuliwa na Marekani dhidi ya kampuni za Kichina ni kitendo cha shinikizo halisi la kisiasa.

Hua Chunying alibainisha kuwa China itachukua hatua muhimu kulinda haki na maslahi yake.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *