img

Kundi la kwanza la wakimbizi wa Rohingya lawasili kisiwa cha Bangladesh

December 5, 2020

Serikali ya Bangladesh Ijumaa imetuma kundi la kwanza lenye zaidi wa wakimbizi 1,500 wa Rohingya katika kisiwa kilichojitenga, cha Bhashan Char licha ya licha ya miito ya makundi ya kutetea haki za binadamu ya kusitisha mchakato huo.

Wakimbizi 1,642 walipanda meli saba za jeshi la Bangladeshi katika bandari ya Chittagong kwa safari ya kuelekea Bhashan Char, kulingana na afisa ambaye hakutaka kutajwa kwa majina.

Umoja wa Mataifa umesema wakimbizi hao walikuwa wapewe fursa ya kuamua kwa hiari ikiwa wanataka kuhamia katika kisiwa hicho kilicho kwenye Ghuba ya Bengal.

Kisiwa hicho kinatajwa kuwa na historia ya kukumbwa na mafuriko na kufunikwa na maji wakati wa mvua kubwa. Lakini hivi sasa kimezingirwa ukingo wa kuzuia maji, na jeshi la Bangladesh limetumia takriban dola milioni 112, kujenga nyumba za kutosha, hospitali na misikiti.

Karte Bangladesch Bhashan Char DE

Aidha baada ya wakimbizi hao kuwasili walipewa chakula, na barakao pamoja na kupimwa joto la mwili kama moja wapo ya hatua za tahadhari za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Kikiwa kilomita 34 kutoka bara, kisiwa hicho kiliibuka tena miaka 20 tu iliyopita na tangu wakati huo hakijawahi kuishiwa na watu.

Miundombinu ya kisiwa hicho imejengwa kukidhi mahitaji ya watu wapatao 100,000, huku kukiwa na mamilioni ya wakimbizi wa Rohingya waliokimbia unyanyasaji wa majeshi ya Myanmar wanaoishi katika kambi za wakimbizi huko Cox’s Bazar Bangladesha.

Mkurugenzi wa maendeleo ya miundombinu kwenye kisiwa hicho cha Bhashan Char, Commodore Abdullah Al Mamun Chowdhury, aliwaambia waandishi wa habari kwamba jumuiya ya kimataifa isiwe na wasiwasi juu ya  kuhusu usalama wa wakimbizi hao.

Chanzo: ap

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *