img

JPM akamilisha baraza la Mawaziri

December 5, 2020

Rais Magufuli amekamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri. Hii leo Baraza limetangwaza ambapo jumla ya Mawaziri 21, na kufanya idadi yao kuwa 23.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi amesema pia Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Naibu Mawaziri 23 na Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali.

Pia amewateua wabunge wawili ambao pia amewapa nafasi ya uwaziri.

Katika orodha iliyotangazwa leo baadhi ya mawaziri wamerejea katika nafasi zao, wengine wakipanda kutoka manaibu waziri na kuwa mawaziri kamili.

Kuna sura mpya zilizojitokeza kwenye baraza hilo, halikadhalika baadhi ya mawaziri katika baraza lililopita wakihamishiwa katika wizara nyingine.

Mawaziri waliosalia katika nafasi zao ni Profesa Joyce Ndalichako (Elimu), Dotto Biteko (Madini), Jenista Mhagama (Ofisi ya Waziri Mkuu), Selemani Jaffo (Tamisemi) na George Simbachawene (Mambo ya Ndani).

Wengine waliorejea kwenye nafasi zao ni Mwigulu Nchemba (Sheria), William Lukuvi (Ardhi), George Mkuchika (Utumishi).

Baadhi ya mawaziri wa awamu iliyopita wamerejea lakini wanehamishwa wizara; nao ni Ummy Mwalimu ambaye sasa ni Waziri wa Muungano na Mazingira kutoka Wizara ya Afya na Innocent Bashungwa ambaye sasa ameteuliwa kuongoza wizara ya Habari na Michezo akitoka Wizara ya Viwanda.

Waliokuwa Manaibu Mawaziri na sasa wamepanda na kuwa Mawaziri kamili ni Dkt Damas Ndumbaro (Maliasili na Utalii), Dkt Faustine Ndungulile anayesimamia wizara mpya (Mawasiliano na Teknolojia) na Juma Aweso (Maji).

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *