img

Haji Manara awachokoza tena mashabiki wa Yanga

December 5, 2020

Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara amewachokoza tena mashabiki wa Klabu ya Yanga ambao walienda kuwapokea wachezaje wa timu ya Plateau United kutoka nchini Nigeria, kwa kusema aliyechukua simu ya mchezaji wa timu hiyo airudishe.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Haji Manara ameandika kuwa “Hivi ilikuaje hasa, aliyechukua simu ya mchezaji wa Plateau United ‘Airport’ arudishe, tuepuke aibu kwa wageni”.

Haji Manara amekuwa aki-trend mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuanzia siku ya Disemba 2,  baada ya kauli yake kuleta utata kuhusu mashabiki wasiokuwa wa Simba wasiende uwanjani.

Siku ya leo kuna mchezo wa marudiano raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Africa kati ya Simba dhidi ya Plateau United utakaochezwa saa 11:00 Jioni uwanja wa Benjamin William Mkapa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *