img

Wanadiplomasia wa juu wa Jordan, Israel wafanya mkutano wa nadra kuhusu suala la Palestina

December 4, 2020

Waziri wa mambo ya kigeni wa Jordan Ayman Safadi amefanya mkutano wa nadra na mwenzake wa Israel Gabi Ashkenazi ili kushinikiza kuanza upya kwa mazungumzo yaliyokwama kati ya Palestina na Israel. 

Mkutano huo wa jana Alhamisi umekuja siku kadhaa baada ya kiongozi wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahmud Abbas kuzuru Jordan, kama sehemu ya ziara yake katika mataifa ya kiarabu kuhamasisha uungwaji mkono kwa msimamo wa Palestina baada ya rais mteule wa Marekani Joe Biden kumshinda Donald Trump kwenye uchaguzi. 

Kwenye mkutano huo, Safadi amenukuliwa na shirika la habari la Petra akisema uundwaji wa taifa huru la Palestina lilikuwa ni suala la muhimu zaidi katika kumaliza mzozo na Israel na kuongeza kwamba hakuna mbadala wa suluhu ya mataifa mawili kati ya Israel na Palestina.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *