img

Virusi vya corona: Biden awataka Wamarekani kuvaa barakoa kwa siku 100

December 4, 2020

Dakika 3 zilizopita

Joe Biden, 3 December 2020

Rais mteule wa Marekani amesema atawaomba raia wa Marekani kuvaa barakoa siku 100 za mwanzo za utawala wake ili kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.

Amezungumza hayo katika kituo cha habari cha CNN, anasema anaamini kuwa itasaidia maambukizi ya corona kupungua kama kila Mmarekani atavaa barakoa.

Bwana Biden alisema pia kuwa atatoa amri katika majengo yote ya serikali watu wavae barakoa.

Marekani ina rekodi ya maambukizi ya corona milioni 14 na vifo vinavyotokana na ugonjwa ni 275,000.

Biden amesema nini kuhusu barakoa?

Katika mahojiano aliyoyafanya na Jake Tapper wa CNN, bwana Biden alisema: “Siku ya kwanza nitakayoapishwa nitawaomba wananchi kuvaa barakoa kwa siku 100 na sio milele.

“Na nadhani itaweza kusaidi kupunguza maambukizi kwa kiasi kikubwa sana, kama chanjo na barakoa zitaweza kupunguza maambukizi.” 

Wataalam wa katiba wanasema rais wa Marekani hana mamlaka ya kutoa amri kwa watu kuvaa barakoa lakini bwana Biden alisema wakati wa mahojiano hayo kuwa makamu wake wa rais Kamala Harris ataweka mfano wa namna ya kufunika uso.

Mamlaka ya rais yanahusisha kulinda mali za serikali ya Marekani, na bwana Biden aliiambia CNN kuwa ana lengo la kutumia mamlaka hayo.

“Ninaenda kutoa agizo katika serikali ya shirikisho kuwa wanapashwa kuvaa barakoa,” alisema.

Aliongeza: “Katika upande wa usafirishaji,kila mtu anapaswa kuvaa barakoa kwenye ndege na mabasi na usafiri wowote.”

Ndege za Marekani , uwanja wa ndege na maeneo mengi ya umma tayari yanawataka abiria na wafanyakazi wake kuvaa barakoa.

White House ya Trump imekataa kufuata agizo hilo kutoka kwa wataalamu wa afya .

Dkt Fauci aliiambia BBC : "Ninaimani kubwa kuhusu kile Uingereza inachokifanya kisasyansi na katika msimamo wake wa udhibiti wa janga"
Maelezo ya picha,

Dkt Fauci aliiambia BBC : “Ninaimani kubwa kuhusu kile Uingereza inachokifanya kisasyansi na katika msimamo wake wa udhibiti wa janga”

Alizungumza huku Gavana wa California Gavin Newsom akitoa amri ya kukaa nyumbani kwa sehemu kubwa ya wakazi wa jimbo lake , akisema ana weka ”mapumziko ya dharura ” huku wagonjwa wa virusi wakitishia kupita uwezo wa hospitali .

Jumatano, Meya wa Los Angeles Eric Garcetti alitoa amri ya kuzuia umma kusafiri kwa miguu au kwa magari, akiongeza kuwa “ni muda wa kuahirisha kila kitu.”

Awali Alhamisi, katika mahojiano na BBC, Dkt Fauci aliomba msamaha kwa maneno ya ukosoaji aliyoyotoa kuhusu mchakato wa Uingereza wa kuidhinisha chanjo ya corona.

“Sikumaaninisha kuoneshaudhaifu wowote wa chanjo hata kama matamshi yangu yalisikika hivyo ,” alisema.

Awali Dkt Fauci aliziambia televisheni za Marekani kwamba waangalizi wa viwango wa uingereza ”waliharakisha” kuidhinisha chanjo.

Biden alisema nini kuhusu chanjo?

m

Rais mteule kutoka Democrat alisema kuwa “anefurahia” kutumia chanjo hiyo mbele ya umma ili kuondoa hofu yoyote kuhusu usalama wake.

Marais watatu wa zamani wa Marekani – Barack Obama, George W Bush na Bill Clinton – wamesema kuwa pia wananajiandaa kuchanjwa mbele ya umma ili kuonesha kuwa chanjo hiyo ni salama.

” Watu wamepoteza imani na uwezo wa ufanisi wa chanjo,”Bw Biden alisema , na kuongeza kuwa “Ni muhimu kwa kile atakachofanya rais na makamu rais .”

Makamu wa rais mteule wa Biden Kamala Harris,ambaye aliungana naye katika mahojiano na CNN, alikosolewa na Warepublican mwezi Septemba baada ya kusema kuwa hataiamini chanjo yoyote iliyoidhinishwa na maafisa wa huduma za afya wakati wa utawala wa Trump.

Kituo cha utafiti cha Pew kinasema ni 60% tu ya Wamarekani ambao kwa sasa wanajiandaa kupokea chanjo ya virusi vya corona, hadi 51% walitoa matamshi sawa na ya Bi Kamala mwezi wa Septemba.

Bw Biden anajiandaa kuchukua mamlaka ya urasi huku makampuni makubwa ya dawa yakiwa yamesitisha mpango wa kusafirisha mamilioni ya dozi za chanjo ya corona kwa umma wa Wamarekani.

Pfizer, ambayo inasema chanjo yake ina ufanisi wa kiwango cha 95% katika majaribio ya kliniki , na Moderna,inayosema dozi yake ina ufanisi wa 94% , zote zimetuma maombi kwa taasisi ya udhibiti wa viwango vya Chakula na Dawa nchini Marekani zikiomba kusambaza chanjo hizo nchini Marekan.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *