img

VIDEO: Askari wa JWTZ amuuwa mkewe

December 4, 2020

WATU wawili wamefariki duninia katika matukio tofauti matatu ambayo yamejitokeza katika Mkoa wa Pwani likiwemo la askari wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ kutoka kikosi cha 92 KJ aliyetambulika kwa jina la Daniel Warioba (43) kumuuwa mke wake aitwaye Joyce Ismail ambaye ni mwalimu katika shule ya msingi Ruvu darajani iliyopo Wilayani Kibaha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa  akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake amesema kwamba tukio hilo limetokea leo katika  maeneo ya mlandizi Wilayani Kibaha ambapo mtuhumiwa huyo  kuamua  kumchomachoma na kitu chenye ncha kali  katika sehemu zake mbali mbali za mwili hadi kufariki dunia.

 TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI……USISAHAU KUSUBSCRIBE

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *