img

Ujerumani yataka mkataba mpana wa nyuklia wa Iran

December 4, 2020

Ujerumani imesema hii leo kwamba ni lazima kufikiwe mkataba mpya na mpana zaidi wa nyuklia wa Iran ili kudhibiti mpango wa makombora wa Tehran na kutahadharisha kuwa mpango wa 2015 haujitoshelezi tena. 

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas amesema kwenye mahojiano na gazeti la Ujerumani la Der Spiegel kwamba kunahitajika makubaliano mapya ya nyuklia. 

Ujerumani kwa sasa inashikilia urais wa Umoja wa Ulaya, imesema kunahitajika mkataba huo kwa sababu hawana imani na Iran. 

Waziri Maas amesema matarajio yao ya wazi kwa Iran, ni kwamba hakutakuwepo na silaha za nyuklia wala mpango wa maroketi ya masafa marefu utakaotishia ukanda mzima, na kuongeza kuwa Iran pia ni lazima ifanye jukumu jingine katika ukanda huo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *