img

Ufaransa yaanza msako dhidi ya makumi kadhaa ya misikiti

December 4, 2020

Dakika 5 zilizopita

Congregation in Paris Pantin mosque, now closed by French authorities, 20 Oct 20

Maelezo ya picha,

Mwezi Oktoba Msikiti Mkubwa wa Paris -Grand Mosque wa Pantin, uliamrishwa kufungwa

Maafisa nchini Ufaransa wameanzisha msako katika makumi kadhaa ya misikiti na kumbi za sala zinazoshukiwa kuwa na uhusiano na Waislamu wenye itikadi kali.

Waziri wa mambo ya ndani Gérald Darmanin ametangaza msako huo , akisema kuwa baadhi ya misikiti inaweza kufungwa iwapo itabainika kuwa inachochea “kujitenga”.

Hii inakuja wiki moja kabla ya kutangazwa wazi kwa sheria mpya ya kupambana na itikadi kali.

Msako huu unafanyaika kufuatia mashambulio ya mwezi Oktoba, ambapo waislamu wenye itikadi kali wanalaumiwa kuhusika ,ikiwa ni pamoja na kukatwa kichwa kwa mwalimu wa Ufaransa Samuel Paty.

Katika taarifa kwa wakuuwa usalama wa kikanda iliyoripotiwa na vyombo vya habari vya Ufaransa, Bw Darmanin alisema kuwa kutakuwa na msako maalumu na upelelezi katika misikiti 76 na kumbi za ibada, 16 kati yake zikiwa katika mkoa wa Paris.

Iliagiza “hatua ya haraka ” kuhusu misikiti 18 kati yake, huku msako wa kwanza ukiwa tayari umefanyika Alhamisi.

Katika ujumbe wake wa Twitter alitoa wito wa kuchukuliwa kwa kile alichokiita “hatua kubwa na zisizotarajiwa kukabiliana na makundi yenye itikadi kali “.

Wakaguzi wa majimbo watachunguza ufadhili wao, mawasiliano ya maimamu wao na uwezekano wa shule za Koran kwa watoto wadogo, limeripoti shirika la habari la Reuters.

Mwandishi wa BBC mjini Paris Hugh Schofield anasema mamlaka ya Bw Darmanin hivi yamekosolewa hivi karibuni kutokana na mzozo juu ya unyanyasaji wa polisi nchini Ufaransa na mapendekezo ya sheria ya kulinda utambulisho wa maafisa wa polisi.

‘Sio kusambazwa kwa itikadi kali’

Anwani 76 za misikiti zinazotarajiwa kusakwa na wapelelezi zina maeneo 2,600 tu ya ibada za Waislamu nchini Ufaransa.

Bw Darmanin alisema kuwa ukweli unadhihirisha kuwa “tuko mbali katika kudhibiti hali ya kusambaa kwa itikadi kali ” miongoni mwa Waislamu nchini Ufransa.

Ufaransa ilishitushwa na kukatwa kichwa kwa mwalimu Samuel Paty na kuchomwa vifu kwa watu watatu ambao walikufa katika kanisa kuu la Nice.

Bw Paty aliuliwa baada ya taarifa juu yake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii akionesha vibonzo vya Mtume Muhammad katika darasa.

Mahakama ya juu iliamrisha kufungwa kwa msikiti Mkubwa wa Pantin, baada ya kuchapisha video inayompinga Bw Paty.

Msikiti huo upo katika eneo linalokaliwa na watu wa kipato cha chini katika eneo la kaskazini -mashariki mji mkuu Paris.

Taifa lisilozingatia dini – au laïcité – ni moja ya nguzo muhimu za utambulisho wa taifa la Ufaransa .

Sheria za Laïcité kwamba eneo la umma-iwe madarasa, maeneo ya kazi au maeneo ya wizara -yanapaswa kuwa huru dhidi ya dini.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *