img

TEA yatoa Mil. 120 kuwapatia mafunzo wajasiliamali 422 Sengerema

December 4, 2020

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kupitia Wizara ya Sayansi na Teknolojia imetoa shilingi milioni 120/- kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya wajasiliamali 422 wilayani Sengerema katika Mkoa wa Mwanza

Fedha hizo zimepitia chuo Cha maendeleo ya Wananchi Sengerema (FDC) ambao ndiyo wanatoa mafunzo hayo kwa wajasiliamali hao yanatolewa bure.

Akisoma taarifa ya chuo hicho kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo mkuu wa chuo  Hagai Shilah alisema mafunzo hayo yanayotolewa yamefadhaliwa na Mamulaka ya Elimu Tanzania (TEA) kupitia mradi wa kukuza ujuzi na stadi za kazi (SDF) .

Kupitia mfumo wa kukuza ujuzi(Skills development funds) (SDF)  fedha hizo hutolewa kwa awamu tatu ,ambazo ni awamu ya kwanza 40% awamu ya pili 40%na awamu ya tatu 20% kadri mradi utavyotekelezwa hadi sasa chuo kimepokea awamu mbili za fedha S48,000.

“Tunawaomba wanasengerema wajitokeze kupata mafunzo hayo kwa kuwa yanatolewa bure yatawasaidia kujifunza stadi za kazi na kuendesha maisha yao “alisema  Shilah.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Magesa Mafuru ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye  uzinduzi  wa mafunzo haya  amewataka waliopata  na wanaoendelea kupata  mafunzo hayo  kutumia ujuzi huo ili kuwaletea maendeleo kwenye maisha yao.

Sambamba na hayo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuunda vikundi ili kupata mikipo inayotolewa na Halmashauri ya Sengerema kwa vijana, akina mama na watu wenye ulemavu.

Elizabeth Matayo ambaye ni mlemavu wa ngozi ambaye anapata mafunzo ya Ushonaji kupitia maradi wa (TEA) alisema licha ya kuwa mlemavu wa ngozi mafunzo haya ya yatamsadia kuendesha maisha kwa kuwa  sasa anajua kushona nguo.

Moja wa washikiriki wa mafunzo hayo Naoami Costantin alisema tangua wapate mafunzo haya wameelewa kushona , kudalizi na kushona masweta  na kutoa wito kwa wanasichana kuacha tabia  ya kufanya biashara ya ngono badara yake waje wapate ujuzi kupitia mafunzo haya  na kijikimu kimaisha.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *