img

Sarah amvaa Harmonize baada ya kumuanika mtoto wake “Hongera kwa adoption, ukome kuongopea mashabiki”

December 4, 2020

Muda mfupi baada ya Harmonize kushea picha na ujumbe wa kumtambulisha mtoto wake wa kike Zulekha Kondegirl aliyempata na mwanamke mwingine, mkewe Sarah Michelloti amemjibu kwa kusema Harmonize amejipa mtoto ambaye sio wake.

Kupitia ukurasa wake Instagram Sarah ameandika kuwa “Mungu wangu watu kweli wamevurugwa, mara mbili wamepima DNA ya mtoto bado majibu ni Negative, ila kwa kuwa umeshindwa kupata mtoto umeamua kujipa mtoto asie wako” 

“Hongera kwa adoption, utakua na roho nzuri hukujua jinsi ya kutunza mke sababu ya maovu yako natumai utajua kutunza mtoto, ukome kuongopea mashabiki dah, nimepost hii kwa lugha ya kiswahili kila mtu ataelewa”.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *