img

Neymar atoa ishara ya kucheza timu moja na Messi msimu ujao

December 4, 2020

Dakika 10 zilizopita

Mshambuliaji wa PSG Neymar

Neymar aliwashangaza wengi aliposema kwamba anataka kucheza na Messi tena msimu ujao , muda mfupi baada ya kuisadia PSG kupata ushindi wa 3-1 katika mashindano ya kombe la klabu bingwa Ulaya dhidi ya Man United.

”Kile ninachohitaji sana ni kucheza tena na Linel Messi , ili kuweza kumfurahikia tena uwanjani”, Neymar aliambia chombo cha habari cha ESPN kuhusu mchezaji mwenza wa Barcelona.

”Anaweza kucheza katika nafasi yangu , sina wasiwasi na hilo. Lakini nataka kuungana naye mwaka ujao kwa kweli. Lazima tuhakikishe kwamba hilo linafanyika mwaka ujao”.

Ufichuzi huo unajiri huku kaimu rais wa klabu hiyo Carlos Tusquets akisema kwamba klabu hiyo ingemuuza Messi msimu uliopita.

Mshambuliaji wa Argentina Messi mwenye umri wa miaka 33 aliambia Barcelona kwamba alitaka kuondoka wakati huo na kusema kwamba kifungu kimoja katika kandarasi kilimaanisha kwamba angeweza kufanya hivyo akiwa huru.

Barca ilisema kwamba hilo halikuwa lengo lao na kwamba hawatamruhusu mfungaji wao wa magoli mengi na nahodha kuondoka kwa chini ya £624m.

Kandarasi yake inakamilika msimu ujao ambapo atakuwa huru kuondoka.

Josep Maria Bartomeu alijiuzulu kama rais wa klabu hiyo mnamo mwezi Oktoba huku Tusquest akichukua uongozi kwa muda hadi uchaguzi utakapofanyika mwezi Januari.

”Kiuchumi, ningemuuza Messi katika msimu uliopita, Tusquest aliambia idhaa ya RAC1. Zote kwa mujibu ya utakachohifadhi katika mshahara pamoja na fedha zinazoingia , ingekuwa bora. Lakini hilo ni suala ambalo makocha wangeruhusu na sio kazi yangu”.

Kandarasi ya Messi inakamilika msimu ujao na mwandishi wa kandanda wa Uhispania Guillem Balague, akizungumza na BBC anasema kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo.

Je kuna mpango wa Neymar kuhamia PSG?

Mwandishi wa soka nchini Ufaransa Julien Lauren anasema kwamba fumbo kubwa ni kwamba Neymar aliondoka Barcelona ili kutokuwa katika kivuli cha Neymar na sasa amefikia kiwango cha hata kumuomba kucheza naye pamoja.

kandarsi ya Messi inakamilika Barcelona msimu ujao.

Mchezaji wa Brazil Neymar aliondoka Barcelona kueleka PSG mwaka 2017 kwa dau lililovunja rekodi £200m, licha ya klabu hiyo ya Uhispania kutotaka kumuuza.

Kuondoka katika kivuli cha Messi na kuwa nyota katika klabu nyengine, hatua ambayo ingemwezesha kushinda kombe la klabu bingwa na taji la mchezaji bora duniani Ballons d’Or.

Je kuna mpango wa Messi kujiunga na Neymar

Joan Laporta na Victor Font – wagombea wawili wanaopatiwa kipaumbele kushinda urais wa klabu hiyo wanasema kwamba wanataka Messi asalie katika klabu.

“Messi hamsubiri Mwenyekiti mpya , alisema Balague, ambaye awali ameandika kuhusu hamu ya Manchester City kutaka kumsaini Messi katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo.

Mwenyekiti mpya atalazimika kumshawishi Messi kusalia. Aliwacha ujumbe ulio wazi – Anataka kuondoka . Anataka kuondoka.

Neymar ana mwaka mmoja na nusu uliosalia katika kandarasi yake , hivyobasi kumuondoa PSG kujiunga na Messi katika klabu ya Manchester City, Juventus, Inter Milan au Chelsea haitawezekana.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *