img

‘Museveni hajawi kukutana na mpinzani jembe kama mimi’- Bobi Wine

December 4, 2020

Mgombea urais wa upinzani nchini Uganda ambaye pia ni mwanamuziki, Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine, amesema kuwa rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni hajawahi kukutana na mpinzani kama yeye.

Kyagulanyi amesema hayo wakati anarejelea tena kampeni zake jana Alhamisi maeneo ya Kibuku, Budaka na Manafwa.

Bobi Wine alivalia mavazi ya kujikinga na risasi kwa mara ya kwanza katika kampeni zake na kuwaarifu wafuasi wake kwamba kuanza wakati huo, anazungumza nao kama ‘Bobi Wine’ wala sio Kyagulanyi kwasababu yeye ni ‘upanga unaokata kote kuwili’.

“Mumemuona Kyagulanyi vya kutosha, sasa ni wakati wa Bobi Wine. Walipofyatulia gari langu risasi wengi walifikiria wakati umewadia wa mimi kusitisha kampeni zangu. Huu ni upanga unaokata kote kuwili. Na sasa ninajitokeza kama Bobi Wine,” mgombea huyo wa chama cha NUP alisema.

”Katika kipindi chake chote cha uongozi, miaka 34, Museveni hajawahi kukutana na mpinzani kama mimi na hii ndio sababu uongozi wake umeingiwa na wasiwasi,” Bobi Wine alisema.

Aidha, Bobi Wine aliongeza, ‘Rais Museveni ana siku 40 pekee za kuwa madarakani na kumuhesabia siku hizo imeanza Desemba 4 ambazo zinaisha siku ya kupiga kura Januari 14, 2021.

Bobi Wine, pia katika kampeni yake, aliahidi Uganda mpya ambapo wahudumu wa afya watapewa kipaumbele na kupewa nyongeza ya mshahara hasa wakati nchi inapokabiliana na janga kama la virusi vya ugonjwa wa corona.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *