img

Mkataba wa kinyuklia: Iran yakataa masharti ya Joe Biden kufufua makubaliano hayo huo

December 4, 2020

Dakika 1 iliyopita

Kituo cha kinyuklia cha Iran

Iran haitakubali masharti mapya kutoka kwa utawala wa rais mteule wa Marekani Joe Biden kuhusu mpango wa kinyuklia na kwamba Marekani ni sharti irudi katika meza ya makubaliano ya 2015 kabla ya mazungumzo kufanyika , imesema wizara yake ya masuala ya kigeni.

Javad Zarif amesema kwamba Marekani ina masharti yake ambayo ni sharti yatekelezwe. Rais Mteule Joe Biden amesema kwamba atairudisha Marekani katika meza ya majadiliano ya mkataba wa kinyuklia na kuondoa vikwazo dhidi ya Tehran itakapofuata makubaliano ya mkataba huo.

Pande zote mbili zinaonekana kutaka upande mwengine kufuata masharti ya makubaliano hayo kwanza. Mnamo mwezi Mei 2018 , rais wa Marekani Donald Trump alijiondoa katika mkataba huo uliojadiliwa na mtangulizi wake Barrack Obama.

Baadaye aliiwekea vikwazo vikali vya kiuchumi Iran , vikilenga mafuta ya taifa hilo na sekta za kifedha. Tehran imepitisha viwango vya mpango wake wa kinyuklia na hivyobasi kuzua wasiwasi kwamba huenda inatumia mpango huo kama sababu ya kutengeneza bomu la kinyuklia.

Serikali yake insisitiza hatahivyo kwamba lengo lake la kinyuklia ni la amani.

Mpango huo uliundwa kukandamiza mradi huo kwa lengo la kulipunguzia vikwazo taifa hilo.

Je msimamo wa Iran ni upi kuhusu mpango wa kinyuklia.

Akihutubia mkutano kupitia mtandao ulioandaliwa na Itali siku ya Alhamisi , bwana Zarrif alisema kwamba Marekani imekuwa ikikiuka makubaliano ya UN kwa kuondoka katika makubaliano hayo wakati wa utawala wa Trump alioutaja kuwa ‘mbaya’ .

”Marekani ni sharti kukoma , Marekani inapaswa kukoma kukiuka sheria za Umoja wa Mataifa” , alisema.

Hatua hiyo aihitaji majadiliano. Bwana Zarrif aliendelea kusema kwamba Marekani haipo katika nafasi ya kuweka masharti.

Bwana Biden, ambaye anakaribia kuapishwa kama rais wa 46 wa Marekani tarehe 20 Januari, alisema kwamba atapatia kipao mbele kuirudisha Marekani katika makubaliano hayo na kujaribu kuondoa vikwazo , lakini Iran italazimika kuafikia masharti hayo

Aliambia gazeti la The New York Times wiki hii kwamba itakuwa vigumu lakini kitu cha mwisho katika eneo hilo la dunia nikujenga uwezo wa kinyuklia “.

Jumatano , bunge la Iran lilipitisha muswada ambao ungezuia maafisa wa uchunguzi wa UN kuzuru katika kituo chake cha kinyuklia na kuipatia ruhusu serikali kuendelea kujilimbikizia madini ya Uranium hadi asilimia 20 ambayo ni zaidi ya kiwango cha asilimia 3.6 kinachohitajika chini ya makubaliano hayo iwapo vikwazo havitaondolewa katika kipindi cha miezi miwili.

Madini ya Uranium yalioboreshwa kwa kiwango cha juu zaidi yanaweza kutumika katika kutengeza bomu la nyuklia, ingawa iwapo imeafikia 20% , ni rahisi kwa teknolojia hiyo kufikia kiwango hicho cha usafi.

Kwanini viwango vya kujilimbikizia madini ya Uranium ni muhimu?

Rais Hassan Rouhani alisema kwamba anapinga utekelezwaji wa sheria hiyo huku kiongozi wa kidini Ayatollah Khamenei akiwa anapaswa kuweka wazi msimamo wake kuhusu muswada huo.

Picha za setlaiti zikionesha kiuo cha kinyuklia cha Natanza huko Isfahan Iran
Maelezo ya picha,

Picha za setlaiti zikionesha kiuo cha kinyuklia cha Natanza huko Isfahan Iran

Picha…A satellite image shows Iran’s Natanz nuclear facility in Isfahan, Iran, 21 October 2020

image captionA satellite image of Iran’s Natanz nuclear facility, one of the sites that could boost uranium enrichment

Hatua hiyo inajiri baada ya mauaji yaliomlenga mwanasayansi mkuu wa Iran kuhusu masuala ya Kinyuklia, Mohsen Fakhrizadeh, ambaye alikuwa na jukumu muhimu katika mpango wa kinyuklia wa taifa hilo.

Aliuawa katika shambulio ambalo halijulikani aliyelitekeleza mjini Tehran siku ya Ijumaa.

Iran inaamini kwamba Israel pamoja na kundi moja la upinzani lililopo mafichoni walitumia silaha inayodhibitiwa na rimoti ili kutekeleza mauaji hayo.

Israel haijazungumzia kuhusu madai hayo kuhusu kuhusika kwake.

Wakati rais Trump alipojindoa katika makubaliano hayo ya kinyuklia, alisema kwamba anataka kuilazimu Iran kuketi chini katika meza ya mazungumzo ili kuweka makubaliano mapya yatakayozuia mpango wake wa kinyuklia mbali na kuizuia kuunda makombora ya masafa marefu.

Iran ilikataa na kufikia mwezi Julai 2019 ilikiuka kiwango cha asilimia 3.6 kuhusu kujilimbikizia madini ya uranium.

Kiwango chake cha Uranium kimeongezeka na kufikia asilimia 4.5 tangu wakati huo. Tehran ilitangaza mwezi Januari kwamba haitafuata masharti ya makunaliano ya mkataba huo.

Ilisema kwamba haitafuata masharti ya kuafikia viwango kuhusu uwezo wake wa kuzalisha madini ya Uranium.

Mwezi uliopita , Shirika la kimataifa la kusimamia nguvu za atomiki lilisema kwamba Iran ilikuwa na zaidi ya mara 12 ya kiwango cha madini ya Uranium kinachohitajika chini ya makubaliano hayo.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *