img

Maambukizi malaria yapungua Afrika

December 4, 2020

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema maambukizi ya malaria yanaendelea kupungua, hasa katika nchi zenye mzigo mkubwa barani Afrika.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema, “ni wakati wa viongozi kote Afrika na ulimwengu kuinuka tena kukabiliana na changamoto ya malaria, kama vile walivyofanya wakati walipoweka msingi wa maendeleo yaliyopatikana tangu mwanzoni mwa karne hii.” Kwa mujibu wa WHO, viongozi wa Kiafrika walitia saini azimio la kihistoria la Abuja wakiahidi kupunguza vifo vya malaria barani Afrika kwa asilimia 50 katika kipindi cha miaka 10.

Mwaka wa 2019, jumla ya maambukizi ya malaria yalikuwa milioni 229 duniani.

Ugonjwa huo uliua watu 409, 000 mwaka jana ikilinganishwa na watu 411,000 mwaka 2018.

Ripoti ya WHO inaeleza kuwa kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma, kanda ya Afrika imebeba zaidi ya asilimia 90 ya mzigo wa magonjwa.

“Tangu mwaka 2000, ukanda huo umepunguza idadi ya vifo vya malaria kwa asilimia 44 kutoka wastani wa watu 680,000 hadi 384 000 kila mwaka. Hata hivyo, maendeleo yamepungua katika miaka ya hivi karibuni, hasa katika nchi zilizo na mzigo mkubwa wa ugonjwa.

“ Upungufu wa fedha katika viwango vya kimataifa na vya ndani unaleta tishio kubwa kwa faida ya baadaye. Katika mwaka 2019, fedha za ufadhili zilifikia Dola3 bilioni za Marekani badala ya Dola 5.6bilioni. Uhaba wa fedha umesababisha upungufu mkubwa katika upatikanaji wa zana zilizothibitika za kuweza kuidhibiti malaria.”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *