img

KMC, Dodoma Jiji kuonyeshana ubabe leo

December 4, 2020

UONGOZI wa KMC umeweka wazi kwamba unatambua ubora wa wapinzani wao Dodoma Jiji ila watapambana kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa leo utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.

KMC ikiwa nafasi ya 8 na pointi zake 18 inakutana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 9 na pointi zake ni 16 imesema itacheza pira mapato na pira kodi ndani ya dakika 90.

Kikiwa chini ya Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na Habibu Kondo ambaye ni msaidizi kitapambana na Mbwana Makata ambaye aliipandisha Dodoma Jiji ndani ya Ligi Kuu Bara.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala ameweka wazi kwamba wanawatambua wapinzani wao namna walivyo imara jambo ambalo linawafanya waingie ndani ya uwanja kwa tahadhari katika kusaka pointi tatu muhimu.

“Tunawafahamu wapinzani wetu kuwa ni wazuri, tunawafuatilia katika michezo yao, lakini pia tuna kiwango kizuri na bora kimchezo na  ushindi kwenye mchezo huo upo ndani ya uwezo wetu, hivyo mashabiki na wapenzi wa KMC FC wategemee kupata burudani safi.

“Mbali na burudani mashabiki wajitokeze kuona Pira Spana, Pira Kodi, Pira Mapato  katika uwanja wetu wa nyumbani,” amesema.

Mchezo huo utachezwa leo Desemba 4, saa 10:00 jioni.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *