img

Boom XB-1 : Ndege mpya ya abiria inayoweza kusafiri kwa kasi zaidi ya sauti

December 4, 2020

 “Watu mara kwa mara wametaka kusafiri kwa haraka , tangu mtu wa kwanza kusafiri katika mabonde kwa kutumia farasi , anasema Mike Bannister.

Bwana Bannister alisafiri kwa kutumia ndege ya Concorde kupitia kampuni ya ndege ya British Airways kwa takirban miaka 22.

Kama rubani mkuu wa ndege hiyo aliendesha ndege hiyo juu ya anga ya London mwezi Oktoba 2003 huku safari yake ya mwisho ikiwa ile alipotua na ndege hiyo katika makavazi ya Bristol.

Karibia miongo miwili baadaye ulimwengu unakaribia kuwa na ndege ya abiria inayoweza kusafiri kwa kasi zaidi ya kasi ya sauti.

Mwezi Huu , kampuni ya ndege ya Boom Supersonic ilianza kufanyia majaribio ndege yake aina ya XB-1 Supersonic.

Ndio ndege ya kwanza aina ya Supersonic ya raia tangu ndege ya Urusi ya Tupolev TU -144 mwaka 1968. Ndege hiyo nyembamba itajaribiwa.

Inatarajiwa kubeba kati ya abiria 65 na 88 kupitia njia za anga ya bahari. Shirika la Nasa lina ndege za kushangaza zaidi zenye mabawa madogo.

Hii itapaa mnamo 2022, ikifuatilia tuzo ya ndege endelevu zaidi.

Pia kuna kamapuni ya kutengeneza ndege ya Aerion, inayosema kwamba aina yake ya ndege itatoa ndege yenye kasi zaidi kufikia mwisho wa muongo huu.

Lakini ikiwa na uwezo wa kubeba kati ya abiria 8 hadi 10 ndege hiyo ya AS2 inalenga soko tofauti ya baishara ya usafiri wa anga za juu .

Bwana Bannister anasema kwamba ni muhimu kuelewa kwamba ndege hizo hazina upinzani bali ujio mpya katika sekta tofauti ya biashara ya usafiri wa ndege.

Shida moja ya uhandisi ambayo ndege hizi zote zinapaswa kukabiliana nayo ni jinsi zitakavyoingiza hewa katika injini kwa kasi kubwa.

Kuvuta hewa kwa kasi ya hali ya juu kunasababisha matatizo kwa injini zote za ndege.

Uingizaji huo umebuniwa ili kuvunja utiririshaji huo wa hewa na kuipunguza kasi ambayo injini inaweza kukabiliana nayo.

Ni eneo nyeti sana, ambalo hata lilisababisha mgogoro wa England na -Ufaransa wakati wa Concorde.

Kampuni ya ndege ya Air France ilisitisha usafiri wa ndege zake , lakini kampuni ya ndege ya Britrish Airways iliendelea na safari zake.

Sababu moja ambayo Airbus ilikuwa na usimamizi wa ndege za Concorde ni kwamba haikutoa mtindo kamili wa jinsi ndege hizo zinavvyoendeshwa kwasbabu mfumo wake wa kuvuta hewa ulikuwa wa siri, anasema Bannister.

Sekta ya anga iko katika mtikisiko mkali kwa sasa, unaosababishwa na janga la Covid-19. Mashirika ya ndege yamechelewesha au kughairi maagizo kwa kukabiliana na kupungua kwa idadi ya abiria.

“Swali kubwa ni jinsi safari za anga zitakavyokuwa baada ya Covid. Kuna nadharia kwamba safari ya biashara haitarudi katika kiwango chake cha awali. Lakini kwa watu matajiri sana hali hii ni muhimu anasema Bw Bannister.

Anafikiri kuwa ndege ziendazo kasi zitaiba abiria kutoka kwenye ndege za kawaida za kibiashara.

Ndege ya Aerion AS2 inatengenezwa mjini Florida karibu na Cape Canaveral.

Kampuni hiyo inasema kuwa ndege ya biashara yenye injini tatu, ambayo itachukua watu wachache ulimwenguni kwa kasi ya 1,000mph, ndio wasafiri wa shughuli za biashara wanaisubiri.

Kampuni inalenga kuirusha ndege hiyo ifikapo mwaka 2027.

Aerion ilijijengea uaminifu wakati kampuni kubwa ya anga ya Boeing ilipoingia na wachache kuwa washirika wa kampuni hiyo, wakichukua viti viwili kwenye bodi ya Aerion.

Vivyo hivyo Boom inajivunia watendaji wa zamani kutoka kwa mkandarasi wa ulinzi Lockheed Martin kwenye bodi yake ya ushauri.

”Si suala la iwapo, ni suala la lini,” anasema Chad Anderson, rais wa Jetcraft, inayonunua, kuuza na kutoa ushauri kuhusu ndege binafsi.

“Jambo lenye thamani tulilonalo sasa ni muda.” Amesema kuwa safari ya kutoka London kwenda New York au Dubai zinafaa kwa teknolojia hii.

Lakini licha ya nia ya Boom ya kuruka juu ya bahari na imani ya Aerion kwamba ndege za Mach 1.4 zinaweza kuvumiliwa nchi kavu, Mamlaka za Marekani bado hazijaondoa marufuku ya kusafiri kwa raia kutumia ndege hiyo iendayo kasi

Kwa hivyo kuna ushawishi wa kisiasa unaopaswa kufanywa ulimwengu mzima na ndege ya X-59 ya Nasa itashiriki kwa kiasi kikubwa katika hii.

Muhimu, ushiriki wa majina makubwa kama vile mtengenezaji wa injini GE na Boeing amegeuza uelekeo baada ya miaka ya nyuma ya ubunifu wa kubahatisha wa ndege ziendazo kasi “Hawa ni watendaji wa kweli, wenye uwezo,” anasema Bw Anderson.

Nasa inahisi kuwa kuongezeka kwa kelele bado ni changamoto kubwa katika kuzifanya ndege hizo za abiria zinazokwenda kasi kuweza kusafiri tena.

Ndege ndefu ya mabawa ya pembe tatu yaliyowekwa sehemu ya mbele za ndege na mkia pamoja na chumba cha ndege cha rubani kando ya pua, X-59 inadhihiridha teknolojia inayokua ambayo itashuhudia abiria wengi wakiongezeka baadaye .

Ikitarajia kuruka mwaka 2022 muundo wake utalazimika kudhibiti kelele ili kupunguza athari inapokuwa ikielekea chini.

Kamera za hali ya juu ni sehemu ya mahitaji kwasababu rubani anahitaji kuona kupitia kwenye pua ndefu .

Ubunifu huu unapaswa kumridhisha Bwana Bannister. Na muonekani wa X-59 na XB-1 kunaacha ndege ya Concorde kuwa mshindi kwa muonekano wake uzuri wake uliundwa kiasi cha kupendwa hadi leo. “Concorde imetimia pande zote za ubongo, kisanii na kisayansi,” rubani mkongwe wa ndege ya Concorde anahitimisha.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *