img

Biden awataka Wamarekani kuvaa barakoa kwa siku 100

December 4, 2020

Rais mteule wa Marekani amesema atawaomba raia wa Marekani kuvaa barakoa siku 100 za mwanzo za utawala wake ili kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.

Amezungumza hayo katika kituo cha habari cha CNN, anasema anaamini kuwa itasaidia maambukizi ya corona kupungua kama kila Mmarekani atavaa barakoa.
Bwana Biden alisema pia kuwa atatoa amri katika majengo yote ya serikali watu wavae barakoa.
Marekani ina rekodi ya maambukizi ya corona milioni 14 na vifo vinavyotokana na ugonjwa ni 275,000.
Biden amesema nini kuhusu barakoa?
Katika mahojiano aliyoyafanya na Jake Tapper wa CNN, bwana Biden alisema: “Siku ya kwanza nitakayoapishwa nitawaomba wananchi kuvaa barakoa kwa siku 100 na sio milele.
“Na nadhani itaweza kusaidi kupunguza maambukizi kwa kiasi kikubwa sana, kama chanjo na barakoa zitaweza kupunguza maambukizi.” 
Wataalam wa katiba wanasema rais wa Marekani hana mamlaka ya kutoa amri kwa watu kuvaa barakoa lakini bwana Biden alisema wakati wa mahojiano hayo kuwa makamu wake wa rais Kamala Harris ataweka mfano wa namna ya kufunika uso.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *