img

Askari atuhumiwa kumuua mkewe, naye anywa sumu

December 4, 2020

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Daniel Warioba anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe, Joyce Islamim (35) ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi  Ruvu darajani.

 Akizungumza leo Ijumaa Desemba 4, 2020 Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyogesa amesema  Warioba (43) wa kikosi cha 92 KJ amefanya kitendo hicho leo alfajiri.

Amesema mtuhumiwa baada ya kumchoma kisu mkewe maeneo mbalimbali mwilini alikunywa sumu kwa lengo la kujiua lakini alikamatwa na kupelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.

 “Hili tukio limetokea saa 10 alfajiri eneo la Janga Mlandizi Kibaha vijijini na chanzo  bado tunaendelea kukichunguza,” amesema Nyigesa.

Katika tukio jingine,  kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Bolizozo anatuhumiwa kumuua mwajiri wake Halima Pwipwi (50)  kwa kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili.

Kamanda huyo amesema baada ya kijana huyo kutenda kosa hilo alikimbia lakini alikamatwa.

Amesema katika halmashauri ya Chalinze, Issa Mwakilasi (40)  mwalimu wa shule ya sekondari Matipwili amejeruhiwa na moto baada watu wasiojulikana kuchoma nyumba anayoishi ambayo ni mali ya shule hiyo.

Amesema moto huo ulidhibitiwa na kwamba mali zilizoteketea ni za thamani ya Sh235,000.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *