img

Afrika ni mbadala wa Mashariki ya Kati katika mapambano dhidi ya makundi ya Jihadi?

December 4, 2020

Dakika 16 zilizopita

Wanajeshi wa Uingereza wamekuwa kwenye mafunzo kujiunga na majeshi ya UN nchini Mali

Karibu wanajeshi 300 wa Uingereza wamewasili katika nchi iliyo Afrika Magharibi , Mali wakati ambapo ni eneo kitovu cha kundi la wanamgambo wa Kiislamu (IS) likionekana kuhamia kutoka Mashariki ya Kati kwenda Afrika.

Katika operesheni ya miaka mitatu ya Newcombe, wanajiunga na kikosi cha karibu wanajeshi 15,000 wa UN , wakiongozwa na Wafaransa, katika juhudi za kusaidia kurejesha usalama wa eneo hilo linalojulikana kama Sahel

Mali ni moja wapo ya mataifa kadhaa ya Sahel ambayo kwa sasa yanapambana na waasi wa jihadi.

Kulingana na Ripoti ya masuala ya Ugaidi Ulimwenguni iliyochapishwa mnamo 25 Novemba, kituo cha kundi la wanamgambo wa Kiislamu IS kimehama kutoka Mashariki ya Kati kwenda Afrika na kwa kiwango fulani Asia Kusini, na vifo kutokana na IS katika eneo la Kusini mwa jangwa la Sahara ni 67% katika kipindi cha mwaka jana.

“Kupanuka kwa washirika wa ISIS katika eneo la Kusini mwa jangwa la Sahara kulisababisha kuongezeka kwa ugaidi katika nchi nyingi kwenye eneo hilo, kwa mujibu wa ripoti inayoangazia masuala ya ugaudi ya Global Terrorism Index.

“Nchi saba kati ya 10 zilizo na ongezeko kubwa la ugaidi zilikuwa Kusini mwa Jangwa la Sahara: Burkina Faso, Msumbiji, DRC, Mali, Niger, Cameroon na Ethiopia”.

Ripoti hiyo inasema kwamba mwaka 2019 “eneo la kusini mwa jangwa la Sahara liliripotiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya vifo vitokanavyo na ugaidi vinavyohusishwa na ISIS vipatavyo 982, au asilimia 41 ya vifo”.

Awamu ijayo ya vita dhidi ya ugaidi’

Wapiganaji wa jihadi kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya kazi barani Afrika.

Katika nyakati za sasa kiongozi wa al-Qaeda marehemu Osama Bin Laden aliifanya Sudan kuwa kituo chake kabla ya kurudi Afghanistan mwaka 1996.

Harakati za Boko Haram za Nigeria, maarufu kwa utekaji nyara dhidi ya mamia ya wasichana wa shule huko Chibok mnamo 2014, walitekeleza mashambulio makubwa baada ya kutangaza jihadi mnamo 2010.

Lakini leo, wakati ushindani ukiongezeka kati ya vikundi hasimu vya jihadi, tishio la ugaidi katika ukanda huo linaongezeka.

Mratibu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani wa kukabiliana na ugaidi, balozi Nathan Sales, anasema IS na al-Qaeda wamehamisha shughuli zao nyingi kutoka Syria na Iraq kuelekea kwa washirika wao huko Magharibi na Afrika Mashariki, na vile vile Afghanistan.

”Afrika”, anasema, ”ni muhimu katika awamu ijayo ya vita dhidi ya ugaidi”.

Mwanajeshi wa Mali akiwa kwenye doria

Nchi gani zilizokithiri?

Mataifa kadhaa masikini zaidi duniani yanapakana na jangwa la Sahara.

Ukanda huu unajulikana kama “Sahel”, neno la Kiarabu linalomaanisha “pwani”.

Mali, Chad, Niger, Burkina Faso na Mauritania zinaunda nchi za Sahel na zote zimepata mashambulio kutoka kwa wanamgambo.

Sehemu za ukanda huo zinakumbwa na ukame, umaskini, ukosefu wa ajira na ufisadi

“Afrika Magharibi”, anasema balozi Sales “ni dhoruba kamili, mataifa yakiwa hayadhibiti mamlaka zao, vikozi vyao hufanya dhuluma, na wana mipaka iliyo inayoingiliwa kirahisi”.

Kikundi kikubwa cha jihadi katika eneo hili ni mshirika wa al-Qaeda Jama’at Nusrat Al-Islam wa’l-Muslimin (JNIM).

Kundi hilo linashindana moja kwa moja na IS linaloshirikiana na (ISGS) na mwaka huu kumeshuhudiwa vita kadhaa kati yao.

Nigeria imekumbwa na mashambulio mabaya zaidi ya jihadi katika eneo hilo, na serikali ikijitahidi kudhibiti Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Kulingana na ripoti ya ugaidi ulimwenguni, Boko Haram imehusika na zaidi ya “vifo 37,500 vinavyohusiana na vita na zaidi ya vifo 19,000 kutokana na ugaidi tangu 2011, haswa nchini Nigeria” lakini pia nchi za jirani.

Boko Haram ilikiri kuwa watiifu kwa IS mwaka 2015

Maelezo ya picha,

Boko Haram pledged allegiance to IS in 2015

Mwaka wa 2015, kikundi kimoja cha Boko Haram kiliahidi utii kwa IS, na kuwa “Islamic State Afrika Magharibi” (Iswap), kuvuka mipaka kwa urahisi na kuteka kituo cha kimataifa katika mwambao wa Ziwa Chad mnamo 2018.

IS imekuwa ikitangaza sana ushirika huu wa Kiafrika.

Mashambulio bado yanachukuliwa kwa jina la Boko Haram. Video iliyochapishwa na kundi hilo tarehe 1 mwezi Desemba ilidai kuhusika na mauaji ya wakulima kadhaa katika jimbo la Borno ambao walidaiwa kushirikiana na vikosi vya serikali.

Mataifa ya Magharibi yametoa msaada mdogo tu wa kijeshi na kiintelijensia kwa Nigeria. Wanadiplomasia wa Magharibi wanasema wanakabiliwa na vikwazo vya ufisadi na rekodi mbaya ya haki za binadamu ya jeshi la Nigeria.

Makosa haya yamekuwa mchango mkubwa katika kutokuamini serikali na kuelekea kuajiri Boko Haram na vikundi vingine vya jihadi katika mkoa huo.

“Pembe ya ufisadi nchini Nigeria” anasema Olivier Guitta, “inaharibu kila kitu”.

Uasi wa Al-Qaeda huko Afrika Kaskazini ulianza nchini Algeria.

Kwa hivyo haishangazi kwamba kiongozi mpya wa al-Qaeda katika Maghreb ya Kiisilamu (AQIM) ni raia wa Algeria.

Mwenye ndevu nyeupe mwenye umri wa miaka 51 Abu Obaida Al-Annabi anachukua nafasi ya mtangulizi wake, Abdelmalik Droukdel, ambaye aliuawa na wanajeshi wa Ufaransa huko Mali mwezi Juni.

Maelfu ya raia wa Tunisia walisafiri kwenda Syria kujiunga na IS

Tunisia, nchi ndogo zaidi katika ukanda huo, ilikuwa na idadi kubwa zaidi ya wajitolea – 15-20,000 – ambao walisafiri kwenda Syria kujiunga na IS wakati wa miaka ya 2013-2018.

Kwa ukosefu mkubwa wa ajira na ukaribu na Libya, Tunisia inaendelea kukabiliwa na tishio la ugaidi.

Libya imekuwa katika hali ya machafuko ya vipindi tangu mapinduzi ya nchi za kiarabu mwaka 2011 na kupinduliwa kwa serikali ya Muammar Gaddafi.

Mwisho wa utawala wake haukutoa tu maelfu ya tani za silaha na vilipuzi kutoka kwenye ghala za silaha za serikali, bali pia nyingi zikiwa zinavuka mpaka wa kusini kwenda nchi za Sahel, pia iliruhusu wanamgambo wa IS kupata nafasi mashariki mwa Libya.

Wanamgambo wa al-Shabab wa Somalia – wa Kiarabu kwa “vijana” – limekuwa moja wapo ya makundi na hatari ya jihadi katika barani Afrika.

“Al-Shabab” anasema Nathan Sales, “inajiona kama kundi lenye mafanikio zaidi la al-Qaeda”.

Al-Shabab wamenusurika juhudi za kijeshi kusitisha shughuli zao

Imenusurika na kampeni za kijeshi za pamoja za kimataifa kulisambaratisha bado limeweza kung’ang’ania katika mipaka yake nchini Kenya na Uganda na vile vile kulipua mabomu makubwa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Operesheni maalum za Marekani za uvamizi na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani, uliozinduliwa kutoka nchi jirani ya Djibouti, unawaua mara kwa mara viongozi wa al-Shabab na bado kundi hilo limeweza kuendelea kuwepo.

Kuingia kwa IS katika wilaya ya kaskazini ya Cabo Delgado chini ya bendera ya “IS Afrika ya Kati” (ISCAP), inaweza kuwa mfano wa uasi kamili uliopangwa karibu kabisa kwenye mtandao.

Maafisa wa kukabiliana na ugaidi wanaamini kwamba wanajihadi wanaofanya kazi katika eneo hili lenye utajiri wa gesi nchini Msumbiji wamesajiliwa mtandaoni na wengine kutoka kwa mpaka wa Tanzania na nchi hiyo lakini hasa bila uwepo wa waajiri waliotumwa kutoka Syria na Iraq.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *