img

Wajasiliamali wa mwangukia Mbunge

December 3, 2020

   Na Hamisi Nasri,Masasi 

  WAJASILIAMALI kundi la usafirishaji maarufu kama bodaboda pamoja na mama lishe wilayani Masasi mkoani Mtwara wamemuomba mbunge wa Masasi mjini,Geofrey Mwambe kuona namna ya kuwawezesha kupata mitaji ili kukuza biashara zao na kuweza kuongeza ujira wa kumudu familia zao.

  Wajasiliamali hao waliyasema hayo jana mjini Masasi mkoani hapa wakati walipokuwa wakieleza kero zao mbele ya mbunge wa Masasi mjini, Mwambe ambapo Mbunge huyo alifanya ziara ya kukuta na makundi hayo ili kusikiliza changamoto zao na baadae aweze kuzitafutia ufumbuzi, kikao kilifanyika katika viwanja vya Halmashauri ya mji Masasi

  Jesca Mrope mkazi wa Masasi mfanyabiashara wa chakula (Mama lishe) alisema wao kama wajasiliamali wadogo kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa mitaji ya kuweza kuendesha biashara zao hali inayowafanya washindwa kumudu maisha yao na kulea watoto wao kwa ujumla.

  Alisema iwapo kama wakiwezeshwa kupata mitaji itakayoweza kuinua biashara zao, biashara hizo zitakuwa na wajasiliamali hao watakuwa kiashara na hata vipato vyao vitakuwa na hatimaye kuinua hali za maisha yao ndani ya familia.

   Naye mjasiliamali mwingine ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Shadida alisema yeye ni mama lishe lakini adha kubwa inayoimkabili kwa sasa ni ugumu katika kumudu familia yake hasa katika kuwapatia watoto wake chakula,mavazi na mahitaji mengine ya msingi

  Alisema hali hiyo inatokana na biashara yake kuwa ndogo na hana uwezo wa kupata mtaji wa kukuza biashara hiyo hivyo kipato anachokipata kutokidhi mahitaji ya msingi ya kila siku ndani ya familia yake. 

  “Tunakuomba mbunge wetu wa Masasi utusaidie kutupatia mitaji hata kwa kutupa mikopo ya riba nafuu huko majumbani kweni kwa sasa hata waume zetu siku hizi wanatutegemea sisi wanawake katika kuendesha maisha ya ndani ya ndoa wao mifuko yao imetoboka kwa maana hawana fedha kabisa,”alisema Mama lishe huyo

  Ally Hamisi mwenyekiti wa usafirishaji kituo cha Kaumu mjini Masasi alisema kutokana na changamoto ya ukosefu wa mitaji na mikopo ya ribaa nafuu kwa wajasilimali wanaiomba serikali na mbunge kwa ujumla kuwasaidia kuwepo kwa bandari kavu itakayokuwa ikiwekwa na mizigo na wao kwenda kubeba na kuisafirisha maeneo mbalimbali.

  Kwa upande wake mbunge wa Masasi,Mwambe alisema amepokea ushauri hilo pamoja na changamoto zote na kwamba ofisi ya itafanya kila jitihada katika kuwa na karibu na makundi yote ili kuweza kuyainua kiuchumi.

  “Tunapaswa kuanzisha benki ya watu wa Masasi pekee kwenye hii beki itakuwa ikitoa mikopo kwa wanamasasi tena kwa masharti nafuu sana ukilinganisha na mabenki mengine ambayo bado mikopo yake imekuwa na ribaa kubwa,”alisema Mwambe 

     Alisema ofisi ya mbunge kwa sasa inafikiri mbali zaidi katika kuwasaidia wajasilimali wadogo ikiwemo kuwa na benki ya watu wa Masasi ambayo itakuwa ikitoa mikopo yenye masharti rafiki kwa wajasiliamali lengo kuwainua wajasiliamali.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *