img

Virusi vya corona: Kituo cha afya CDC chatahadharisha wasafiri wanaokwenda Afrika Mashariki

December 3, 2020

Dakika 18 zilizopita

Wasafiri wametakiwa kuchukua tahadhari wanapoingia Afrika Mashariki

Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC) kimetoa tahadhari kwa raia wake kutofanya safari kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki (Kenya, Tanzania, Uganda) kwa kile ilichodai kuwa nchi hizo zina kiwango kikubwa cha maambukizi ya Covid-19, kitaalamu (A Level 4 alert).

‘A Level alert’ ina maana kuwa raia wa Marekani wanapaswa kuepuka kusafiri kwenye nchi hizo kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya Covid-19, kwa mujibu wa tathimini ya CDC.

Tahadhari hiyo imekuja wakati ambapo Marekani imeripoti idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na virusi vya corona kwa siku moja, huku idadi ya vifo kwa siku ya Jumatano pekee ikiwa watu 3,157.

Zaidi ya watu 273,799 wamepoteza maisha kutokana na virusi hivi na zaidi ya watu milioni 13.9 wameambukizwa, kwa mujibu wa takwimu za Chuo cha Johns Hopkins.

Taasisi hiyo ya Marekani imeshauri watu wanaosafiri kuelekea nchi hizo kupima siku moja mpaka tatu kabla ya safari.

”Usisafiri kama unasubiri majibu ya vipimo, ikiwa umekutwa na maambukizi au mgonjwa,” imeongeza CDC.

Wasafiri wa Kimarekani wameshauriwa na CDC ”kuvaa barakoa, kutokaribiana na watu ambao hawasafiri na wewe, onsha mikono yako na mara kwa mara tumia vitakasa mikono , na fuatilia kwa karibu afya yako.”

Na kabla ya kusafiri kurejea Marekani, wasafiri wametakiwa kupimwa na kukaa karantini kwa siku saba baada ya kuwasili nyumbani.

“Usipopimwa, ni salama kukaa nyumbani kwa siku 14. Ikiwa utakutwa na COVID-19 wakati wa kusafiri, ahirisha safari, kaa karantini, fanya vipimo , na uangalie afya yako,” imesema Taasisi ya afya ya Marekani.

Rwanda pekee imetathiminiwa kuwa nchi yenye kiwango cha chini cha maambukizi, hata hiyo wasafiri wametakiwa kufuata taratibu kabla ya kuingia na kutoka nchini humo

Kenya imeripoti maambukizi ya watu 85,130 na vifo 1,484 vilivyotokana na virusi vya corona mpaka sasa

Takwimu rasmi za mwisho za Tanzania zilitangazwa 29 Aprili na Waziri Mkuu ambapo wagonjwa walikuwa 480, na waliokuwa wamefariki kutokana na ugonjwa huo walikuwa 21. Zanzibar baadaye ilitangaza ongezeko la wagonjwa mara moja, mnamo tarehe 7 mwezi Mei walipotangaza wagonjwa 29 wapya.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *