img

Uingereza nchi ya kwanza kuidhinisha chanjo ya Pfizer ya corona

December 3, 2020

Uingereza imeidhinisha chanjo ya COVID19 kutoka Pfizer/BioNTech kwa matumizi ambapo inaweza kuanza kutumika ndani ya siku chache zijazo kwa makundi ya watu waliopewa kipaumbele.

Mamlaka zimesema chanjo hiyo ambayo ni salama kwa asilimia 95 dhidi ya Virusi vya Corona itaanza kutolewa wiki ijayo. Uingereza tayari imeagiza dozi Milioni 40 ambazo zinaweza kutumika kwa watu Milioni 20.

Wataalamu wamesema licha ya uwepo wa Chanjo hiyo, wananchi wanapswa kuendelea kuzingatia tahadhari zilizotolewa ili kudhibiti maambukizi zaidi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *