img

Simba yatoa tamko juu ya ubaguzi wa mashabiki

December 3, 2020

Klabu ya Simba inapenda kutoa taarifa kwa umma kwamba kauli inayoashiria kuzia baadhi ya washabiki wasifike uwanjani kuangalia mchezo kati ya Simba na Plateau United ya Nigeria haikutolewa kwa maelekezo ya klabu.

Kauli hiyo haiwakilishi utamaduni wa kihistoria wa klabu hiyo wa kutobagua wala kubughudhi mashabiki wa timu pinzani wanapokuja kutazama mechi zao.

Taarifa imearifu kwamba tayari wamechukua hatua za kiutawala ndani ya klabu kuhakikisha kwamba suala hilo halitokei tena.

Inafahamika kwamba kadri timu za tanzania zinavyofika hatua za mbele zaidi katika michuano ya klabu bingwa afrika, ndipo nchi yetu inaongeza idadi ya wawakilishi kwenye michuano hiyo kwa msimu ujao.

Kwa msingi huo klabu inaendelea kuwahimiza washabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao kwa maslahi mapana ya mpira wa Tanzania .

Pia klabu ya Simba inapenda kutoa kauli kwamba kama wapo watanzania wenzao ambao wanatamani Simba ikwame mapema katika hatua hii, na nchi isiongeze uwakilishi kwenye michuano ya kimataifa, na kwahiyo wana nia ya kwenda uwanjani kuwashangilia timu za nchi za kigeni, wao kama wenyeji wa mchezo bado wanawahakikishia kwamba hawatozuiwa uwanjani.

Vilevile washabiki hao hawatopata bughudha yoyote kutoka kwa mashabiki wa Simba huku wakiamini kwamba mamlaka husika pia zitahakikisha amani na usalama.

Jambo pekee ambalo klabu ya Simba haiwezi kuwahakikishia mashabiki hawa wa timu pinzani ni kutokupata taibu.

Mpira ni furaha, watanzania wote wanakaribishwa uwanja wa Benjamin William Mkapa siku ya tarehe 5 disemba 2020 saa 11 jioni.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *