img

Shirika la OCODE lapania kuwakomboa watoto wa kike,wakiume katika unyanyasaji wa kijinsia

December 3, 2020

NA VICTOR MASANGU, KIBAMBA

KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na vita dhidi ya  unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike  na wakume Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization for Community Development (OCODE) limekuja na mpango wa  kampeni maalumu ambayo itawasaidia wanafunzi wa shule za awali  na msingi zilizopo  katika manispaa ya Ubungo lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo  katika kupinga  vitendo vya ukatili.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa  Shirika hilo la (OCODE) Joseph Jakson wakati wa  sherehe za ufunguzi wa  kampeni maalumu ya  siku 16 kwa ajili ya  kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike  zilizoandaliwa na shirika hilo kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusiana na vitendo vya  ukatili ambayo imefanyika  katika kata ya kibamba manispaa ya ubungo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa shirika hilo  ambalo lilianzishwa mnamo  mwaka 1999 kwa sasa linatekeleza miradi mbali mbali ya vijana lengo lake kubwa ikiwa ni kusaidia na kuiwezesha jamii kuweza kutambua umuhimu wa elimu bora kuanzia ngazi ya awali pamoja na ile ya msingi kwa watoto na kuwajengea vijana uwezo katika kuboresha masiha yao.

“Shirika letu la Ocode kwa kushirikiana na wadau pamoja na viongozi wa serikali kutoka manispaa ya Ubungo tumeona tumekuwa tukishirikiana bega kwa bega katika miradi yetu mbali mbali lakini kwa wakati huu tupo kwa ajili ya kuungana kwa pamoja kwa ajili ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambayo yanatarajia kufanyika kidunia  disemba 10 mwaka huu,”alisema Mkurugenzi huyo.

Kadhalika aliongeza wameamua kuzitumia siku 16 za  kupinga ukatili wa kijinsia kwa lengo la kuweza kutoa elimu mbali mbali kwa vijana pamoja na wanafunzi kuhusiana na vitendo vya ukatili ili kuweza kuona namna gani ya kuweza kuwapa fursa ya kujitambua na hatimaye kuendelea kuishi kwa misingi ya kupatiwa haki bila uonevu wowote.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya ushauri wa masuala ya afya Dr. Cecilia Mkafu ambaye alikuwa mgeni rami katika halfa hiyo amebainisha kuwa  katika kukabiliana na kujiepusha na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike wanapaswa kuhakikisha wanajiamini na kujitambua pamoja na kupatiwa elimu  ili waweze kutambua  haki zao za msingi.

“Natambua kuna siku 16 za ukatili wa kijinisia ambazo uwa zinaazimishwa kila mwaka kwa hivyo mimi kwa upande wake nalipongeza shirika la Ocode kwa kuweza kutenga siku hii kwa ajili ya kufanya kampeni maalumu ambayo imewashirikisha wanafunzi mbali mbali wa manispaa ya ubungo yote haya ni kwa lengo la kushiriki na kujifunza mambo mbali mbali ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia.

Naye  mmoja wa walimu waliohudhulia hafla hiyo  Amina Muchumu amewaomba wazazi na walezi kuhakikisha kwamba wanaondokana na wimbi la kuwafanyia vitendo vya ukatili na unyanyasaji ya kijinsia watoto wao na badala yake watilie mkazo zaidi katika kuwapeleka shule na kuimba serikali kuwachukulia hatua kali kwa wale watakaobainika wanavunja sheria.

SHIRIKA la Organization for Community Development (OCODE)  ambalo limeanishwa mwaka 1999 limekuwa likishirikiana na serikali kwa hali na mali katika kuisaidia jamii katika masuala ya kuleta maendeleo ikiwemo kuwajengea uwezo vijana pamoja na wanafunzi wa shule za awali na msingi waweze kujitambua katika mambo ya kimaendeleo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *