img

Rais wa zamani wa Ufaransa afariki kwa Covid-19

December 3, 2020

Aliyewahi kuwa rais wa Ufaransa Valery Giscard d’Estaing amefariki dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 akiwa na umri wa miaka 94. Giscard alikuwa mtetezi mkubwa wa hatua ya ujumuishaji wa jamii mbalimbali za watu barani Ulaya aliyeiongoza nchi yake kuingia kwenye enzi mpya.

 Giscard ambaye alipelekwa hospitali mara kadhaa katika miezi ya karibuni kutokana na matatizo ya moyo alifariki jumatano usiku akiwa amezungukwa na familia yake katika makaazi ya kifamilia kwenye eneo la Loire. 

Rais Emmanuel Macron akizungumzia mtangulizi wake huyo amesema miaka yake saba kama kiongozi aliibadilisha Ufaransa na kifo chake kimeitumbukiza nchi hiyo kwenye majonzi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *