img

Rais wa Azerbaijan atangaza Novemba 10 kuwa “Siku ya Ushindi”

December 3, 2020

Rais wa Azerbaijan İlham Aliyev, ametangaza tarehe ya Novemba 10 kuwa “Siku ya Ushindi”, wakati aliposaini tamko la kukubali kushindwa kwa Armenia.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais ya Azerbaijan, Aliyev aliamua kutangaza Novemba 10 kuwa “Siku ya Ushindi” ambayo itaadhimishwa kila mwaka.

Aliyev pia alitangaza tarehe ya Septemba 27 ambayo ni tarehe iliyoanzishwa operesheni za jeshi la Azerbaijan za kukomboa ardhi yake, kuwa “Siku ya Ukumbusho” wa mashujaa.

Armenia ilikiri kushindwa baada ya ukombozi wa vituo 5 vya miji, wilaya 4 na vijiji 286 kufuatia operesheni iliyoanzishwa na jeshi la Azerbaijan na kudumu kwa siku 44.

Armenia ilisaini makubaliano hayo mnamo Novemba 10, na kuahidi kujiondoa kwenye maeneo ya Aghdam, Lachin na Kelbajar.

Gwaride la kijeshi litafanyika katika mji mkuu wa Baku kwa ajili ya ushindi wa jeshi la Azerbaijan.

Hafla hiyo ya gwaride itaandaliwa kwenye uwanja maarufu wa uhuru ulioko katika mji mkuu ambapo kutakuwa na maonyesho ya magari ya kivita na silaha zingine zilizokamatwa na jeshi la Azerbaijan kutoka kwa jeshi la Armenia. Hakuna maelezo rasmi yaliyotolewa kuhusu tarehe ya sherehe hiyo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *