img

Rais Mwinyi “Corona limekuwa kisingizio katika ukusanyaji kodi”

December 3, 2020

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, amesema ugonjwa wa corona umekuwa kisingizio katika ukusanyaji wa kodi licha ya kwamba inaonyesha hakuna jitihada za makusudi kufikia lengo.

Akizungumza juzi Ikulu Zanzibar alipofanya mazungumzo na uongozi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ukiongozwa na Gavana Prof. Florens.

Alisema licha ya kuwapo kwa ugonjwa wa corona, mifumo ya kodi nayo ikikaa sawa mafanikio makubwa yanaweza kupatikana na kutekelezeka.

Dk. Mwinyi alisema uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia kodi na fedha, utasaidia na ni vyema kiongozi huyo akahakikisha katika muda mfupi mifumo inakaa sawa na kwa vile anatokea BoT ana matumaini makubwa kwamba atapata msaada kutoka benki hiyo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *