img

Mwanaume wa Kiislamu akamatwa baada ya kumuoa mwanamke wa Kihindu nchini India

December 3, 2020

Dakika 4 zilizopita

Waandamanaji wanaopinga sheria ya 'jihadi ya mapenzi'

Polisi katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India wamemkamata mwanaume wa Kiislamu kwa madai ya kujaribu kumbadilisha dini mwanamke wa Kihindu kuwa Muislamu.

Yeye ndiye wa kwanza kukamatwa chini ya sheria mpya ya kupinga kubadilishwa ambayo inalenga “jihadi ya mapenzi” – neno linalotumiwa na makundi ya Wahindu kuwatuhumu wanaume Waislamu kwa kuwabadilisha dini wanawake wa Kihindu kwa ndoa.

Sheria hiyo imesababisha ghadhabu, huku wakosoaji wakiita chuki dhidi ya Uislamu.

Takribani majimbo mengine manne ya India yanatunga sheria dhidi ya “jihadi ya mapenzi”.

Polisi katika wilaya ya Bareilly ya Uttar Pradesh walithibitisha kukamatwa kwake kwenye mtandao wa Twitter siku ya Jumatano.

Baba wa mwanamke huyo aliiambia BBC idhaa ya Kihindi kwamba aliwasilisha malalamiko kwa sababu mwanamume huyo “alimshinikiza” binti yake abadili dini na kumtishia ikiwa hatafanya hivyo. Mwanamke huyo anadaiwa alikuwa na uhusiano na mwanaume huyo lakini aliolewa na mtu mwingine mwanzoni mwa mwaka huu.

Polisi waliambia BBC idhaa ya Kihindi kwamba familia ya mwanamke huyo ilikuwa imewasilisha kesi ya utekaji nyara dhidi ya mshtakiwa mwaka mmoja uliopita lakini kesi hiyo ilifungwa baada ya kupatikana na kukanusha shtaka hilo.

Baada ya kukamatwa Jumatano, mwanaume huyo alipelekwa kizuizini kwa siku 14. Aliwaambia waandishi wa habari kuwa hana hatia na “hana uhusiano wowote na mwanamke huyo”.

Sheria mpya inabeba kifungo cha hadi miaka 10 na makosa chini yake hayana dhamana.

Waandamanaji wanaopinga sheria ya 'jihadi ya mapenzi'

Sheria ya ‘jihadi ya mapenzi’ ni nini?

Mwezi Novemba, Uttar Pradesh lilikuwa jimbo la kwanza kupitisha sheria dhidi ya wongofu wa kidini “wa kulazimishwa” au “ulaghai”.

Lakini inaweza kuwa sio ya mwisho kwani takribani majimbo manne – Madhya Pradesh, Haryana, Karnataka na Assam – wamesema kuwa wanapanga kuleta sheria dhidi ya “jihadi ya mapenzi”. Majimbo yote matano yanatawaliwa na chama tawala cha Bharatiya Janata Party (BJP), ambacho kimeshutumiwa kuhalalisha chuki dhidi ya Waislamu.

Wakosoaji wameiita kuwa ya kusumbua na ya kukera, na wengi wana wasiwasi kuwa sheria kama hizo zitatumika vibaya na kuchochea unyanyasaji kwani “jihadi ya mapenzi” imekuwa ikionekana kama neno linalotumiwa na vikundi vya Wahindu wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia. Sio neno linalotambuliwa rasmi na sheria ya India.

Lakini imekuwa ikitawala vichwa vya habari katika miezi michache iliyopita – mwezi Oktoba, chapa maarufu ya vito iliondoa tangazo lililowashirikisha wanandoa wa imani tofauti baada ya kushututumiwa kuunga mkono “jihadi ya mapenzi”.

Kisha mwezi Novemba, mamlaka ziliishutumu Netflix kwa vivyo hivyo, kwa kuonesha onesho la tamthilia ya runinga, ‘A Suitable Boy’, ambapo mwanamke wa Kihindu na mwanaume wa Kiislam wankipigana busu wakati kamera ikielekea nyuma ya hekalu la Kihindu. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Madhya Pradesh, Narottam Mishra, alisema inaumiza “hisia za kidini” na kuamuru maafisa wachunguze na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtayarishaji na mkurugenzi wa tamthilia hiyo.

Wakosoaji wa BJP wanasema ubaguzi wa kidini umeongezeka tangu Waziri Mkuu Narendra Modi alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza mnamo 2014. Ndoa za Wahindu na Waislamu kwa muda mrefu zimesababisha ukosoaji nchini India.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *