img

Matumizi ya nyama za maabara yaidhinishwa Singapore

December 3, 2020

Dakika 3 zilizopita

Eat Just chicken nuggets

Maelezo ya picha,

Eat Just chicken nuggets

Mamlaka ya Singapore imekuwa nchi ya kwanza duniani kuruhusu nyama nyama ambayo haijatoka kwa mnyama aliyechinjwa.

Maamuzi hayo yametoa mwanya wa kuanza kuliwa kwa nyama ya kuku ambayo imetengenezwa katika maabara.

Kampuni ya kutengeneza nyama hizo haijasema zitakuwa tayari lini kuanza kutumika.

Uhitaji wa nyama mbadala unaongezeka kutokana na wasiwasi wa wateja juu ya afya zao ,makuzi ya wanyama na mazingira yanayowazunguka.

Kwa mujibu wa Barclays, soko la nyama mbadala itaweza kuwa na thamani ya dola bilioni 140 (£104bn) ndani ya muongo ujao, au asilimia zipatazo 10 za viwanda vya nyama duniani vyenye thamani ya dola trilioni 1.4tn .

Nyama zinazotegemea mimea zimekuwa na vyakula vingine ambavyo huwezi kuvidhani vimeongezeka katika maduka makubwa pamoja na migahawa mbalimbali.

Lakini kula tu hizi bidhaa ni tofauti kwasababu hazina uhusiano wowote na mimea lakini huwa zinakuzwa katika maabara.

Kampuni ya chakula cha viwandani duniani

Kampuni ya chakula cha viwandani inayoitwa ‘breakthrough ” ina matumaini kuwa mataifa mengine yataanza kufanya kile wanachokifanya.

Zaidi ya muongo mmoja, kuna majaribio kadhaa ya kuleta nyama mbadala sokoni , kukiwa na matumaini ya kupata walaji wengi zaidi na kuandaa bidhaa bora zaidi.

Maeneo mawili makubwa ambayo yako Israel-kuna matumaini ya teknolojia ya nyama za kutengenezwa kupata soko kwa gharama nafuu na ladha nzuri.

Wakati huohuo wengine wakihisi kutakuwa na faida katika mazingira lakini wanasayansi wanahisi teknolojia hii inaweza kusababisha madhara makubwa zaidi katika mabadiliko ya tabia nchi.

Presentational grey line

Mkuu wa kampuni ya ‘Eat Just’ aliuita uvumbuzi huo “moja wapo ya hatua kubwa muhimu katika sekta ya viwanda vya chakula ” lakini changamoto bado ipo.

Kwanza, nyama ya kuku hao ni ghali zaidi kutengeneza-nyama inayotokana na kuku waliokulia katika maabara .

Awali Eat Just ilisema itauza nyama ya kuku wa maabara kwa dola 50 kila mmoja.

Gharama kwa sasa imeshuka, lakini bado ni ghali kutokana na kwamba ni kuku wa kiwango cha juu.

Changamoto nyingine kwa kampuni ni jinsi kuku hao walibyopokelewa na walaji.

Lakini kuidhinishwa kwa bidhaa hii ya Eat Just na Singapore kuna uwezekano wa kuwavutia washindani wengine kuanzisha biashara ya aina hiyo katika miji mingine, na inaweza kuchochea nchi nyingine kuidhinisha nyama hiyo ya kuku ya maabara pia .

Usalama wa ‘chakula kipya’

Shirika la vyakula la Singapore (SFA) limesema kuwa kikundi cha wataalamu kilifanya tathmini ya data kuhusu ulaji wa chakula kilichotengenezwa na kampuni ya Eat Just na kupima usalama wa kuku wa maabara.

” Ilibainika kuwa kuku hao ni salama kwa ulaji kwa viwango vilivyokusudiwa kutumiwa, na waliruhusiwa kuuzwa nchini Singapore kama moja wapo ya bidhaa zilitokana na wazo la thamani au za Eat Just ,” SFA ilisema.

Shirika hilo lilisema kuwa limeweka muundo wa udhibiti wa viwango kwa ajili ya “vyakula vipya “ili kuhakikisha kwamba nyama inayotengenezwa kwenye maabara nap rotini nyinginezo mbadala vinatimiza viwango hitajika kabla ya kuuzwa nchini Singapore.

“Nina uhakika kwamba uidhinishwaji wetu wa nyama inayotengenezwa katika maabara utakuwa ni wa kwanza kati ya wengi nchini Singapore nan chi nyingine kote duniani ,” alisema Josh Tetrick, muasisi mwenza wa Eat Just katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Hakuna dawa za antibiotic zilizotumiwa katika mchakato mzima, na kuku walikuwa na kiwango cha chini cha maikrobaiolojia kuliko kuku wa kawaida, ilisema kampuni hiyo.

“Ni nyama ya kwanza duniani kuruhusiwa na wadhibiti wa viwango , nyama yenye kiwango cha hali ya juu iliyobuniwa kutoka kwa seli ya mnyama kwa ajili ya kuliwa na binadamu ambayo inayoa fursa ya kuanzishwa kwa biashara za kiwango kidogo nchini Singapore siku zijazo,” ilisema kampuni ya Eat Just .

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *