img

Mataifa yapiga kura kutaka kuhalalisha matumizi ya bangi

December 3, 2020

Mkutano wa kila mwaka kuhusu dawa za kulevya, ambao huleta Pamoja maafisa wa umoja mataifa kuhusu dawa na tume inayosimamia uchunguzi wa uhalifu, wamepiga kura jumatano.

Kura 27 zimepigwa kupinga hatua hiyo huku 25 wakiunga mkono. Mtu mmoja aliamua kutopiga kura ya kutaka bangi kuondolewa katika orodha ya dawa za kulevya kulingana na maamuzi namba 4 ya mwaka 1961 ya umoja wa mataifa kuhusu matumizi ya dawa.

Upigaji kura unafuatia maamuzi ya mwaka 2019 ya umoja wa mataifa kwamba bangi inastahili kufanyiwa majaribio ya kimaabara na utafiti kujua kama inaweza kutumika na madaktari kama tiba.

Kulingana na shirika la afya duniani bangi haina madhara makubwa kiasi cha kusababisha kifo na kwamba imeonyesha uwezo mkubwa katika kutibu magonjwa kama kifafa.

Taarifa ya umoja wa mataifa haijasema nchi ambazo zimeunga mkono wala kukataa matumizi ya bangi kwa utafiti wa tiba wakati wa kikao hicho cha Vienna.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *