img

Magufuli asema sherehe uhuru wa Tanganyika 2020 hazitafanyika

December 3, 2020

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema hakutakuwa na sherehe ya uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 2020 na kuagiza fedha zilizopangwa kutumika katika sherehe hizo kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya hospitali ya Uhuru iliyopo jijini Dodoma.

 Agizo hilo la Rais Magufuli limeelezwa leo Alhamisi Desemba 3, 2020 na waziri mkuu, Kassim Majaliwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya chama cha waajiri nchini (Ate).

Majaliwa amesema fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hizo Sh835.4 milioni zitapelekwa katika hospitali ya Uhuru jijini Dodoma kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali.

Amesema hospitali hiyo ilianza kujengwa mwaka 2019 baada ya Rais Magufuli kuagiza fedha zilizotengwa kwenye sherehe za uhuru mwaka 2018  kiasi cha Sh915 milioni kuelekezwa katika ujenzi huo.

“Maadhimisho ya uhuru ya mwaka huu yafanyike kwa kila mmoja kufanya kazi za kijamii katika eneo lake,” amesema Majaliwa na kueleza kwamba serikali iliamua kuipandisha hadhi hospitali hiyo na kupanua ujenzi wake.

Amesema gharama za ujenzi wa hospitali hiyo sasa zimefikia Sh4.2 bilioni baada ya Rais Magufuli kuongeza Sh2.4 bilioni nyingine kwa ajili ya ujenzi huo.

Amebainisha kuwa ujenzi wake mpaka sasa umefikia asilimia 92, “lengo letu tunataka kufikia Desemba 30 mwaka huu, hospitali hiyo ianze kutumika.”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *